Mbwa wanavyomfariji Malkia Elizabeth II

Muktasari:

Kwa sasa Malkia Elizabeth II amejitenga kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona, huku mumewe Prince Phillip akiwa hospitalini baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo.
 

London, Uingereza (AFP)
Malkia Elizabeth II sasa anafarijiwa na mbwa wawili wadogo alionunua katika kip[indi ambacho mumewe, Prince Phillip amelazwa huku mjukuuu wake, Prince Harry na mkewe wameamua kuzungumza kila kitu katika mahojiano yaliyofanyika California nchini Marekani, gazeti la The Sun limeripoti.


Malkia Elizabet amenunua mbwa hao wawili baada ya mbwa wake tofauti kufariki miaka kadhaa iliyopita.
Gazeti hilo limesema mbwa hao waliochangamka-- ambao ni sehemu ya orodha ndefu ya mbwa wanaomuondolea upweke malkia mwenye umri wa miaka 94 -- wanampa furaha wakati huu ambao familia ya kifalme inapitia katika hali ngumu.
Prince Phillip ambaye ana miaka 99 ndio kwanza amefanyiwa upasuaji wa moyo, wakati mjukuu wake mkubwa, Prince Harry na mkewe walifanya mahojiano ya kueleza kila kitu baada ya kuhamia  California.
Mbwa hao wameripotiwa kuwa wanaishi na malkia kwa wiki kadhaa katika jumba lao la Windsor magharibi mwa London, ambako amejitenga kwa karibu mwaka mmoja kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona.
"Malkia amefurahia," limeandika The Sun likimkariri mtu ambaye hakutajwa jina.
"Wote wanasemekana kupiga kelele na kuweka nguvu katika jumba hilo wakati Philip akiwa hospitalini."
Makazi yake katika kasri ya Buckingham Palace hayakutaka kuzungumzia suala hilo. 
Mwandishi wa familia hiyo, Penny Junor aliliambia gazeti hilo kuwa mbwa hao "wanamtii malkia na kumpenda na hawajawahi kumuangusha".
"Na ni dhahiri corgis (mbwa hao) ni nadra sana kwenda LA (Los Angeles) kufanya mahojiano," aliongeza, akionekana kurejea waziwazi kitendo cha Harry na Meghan kufanya mahojiano yaliyokuwa yakisubiriwa sana na Oprah Winfrey na ambayo nyatarushwa Jumapili.
Malkia amekuwa akiwapenda mbwa hao aina ya corgis -- wadogo wenye asili ya Wales na wanaotumika kuchungia -- na wamekuwa karibu sana na wanafamilia ya kifalme.
Duniani, walionekana katika sehemu moja ya filamu ya "James Bond" pamoja na muigizaji Daniel Craig, ambayo ilichukuliwa kwa ajili ya sherehe za ufunguzi za Michezo ya Olimpiki ya mwaka 2012 jijini London.