MCL, Vodacom kutambulisha huduma ya e Gazeti

New Content Item (2)
New Content Item (2)

Muktasari:

  • Kampuni za Mwananchi Communications Ltd (MCL) na Vodacom Tanzania kesho Jumatano Agosti 3, 2022 wanatarajia kutambulisha huduma mpya ya e Gazeti itakayokuwa inapatikana ndani ya My Vodacom App, katika viwanja vya Maonyesho ya Wakulima Nanenane mkoani Mbeya.


Mbeya.  Kampuni za Mwananchi Communications Ltd (MCL) na Vodacom Tanzania kesho Jumatano Agosti 3, 2022 wanatarajia kutambulisha huduma mpya ya e Gazeti itakayokuwa inapatikana ndani ya My Vodacom App, katika viwanja vya Maonyesho ya Wakulima Nanenane mkoani Mbeya.

Akizungumzia maandalizi ya utambulisho huo, Msimamizi wa Biashara za Kidigitali wa MCL, Amir Simbano amesema lengo la huduma hiyo ni kumuwezesha Mtanzania kupata taarifa kwa wakati kupitia simu yake ya mkononi.

“Uzinduzi tutaufanya rasmi baada ya Nanenane lakini tunachofanya sasa ni kuitambulisha tu huduma yetu kwa wakazi wa Mbeya na Nyanda za Juu Kusini  kupitia maonyesho haya, tunataka Watanzania wapate huduma.

“Nawaomba watanzania wachangamkie huduma hii ni rahisi zaidi na itawapatia kile wanachotaka kwa wakati kabisa.” amesema Simbano na kuongeza;

Kwa upande wake, Meneja wa huduma za Kidigitali wa Vodacom Tanzania, Furaha Limu amesema wamekuja na huduma hiyo kutokana na mahitaji makubwa ya wateja wao pamoja na ukuaji wa soko la kidigitali.

“Tumeona tuwarahisishie wateja wetu kupata huduma hii kupitia My Vodacon App, na wataweza kulipa kupitia MPESA na kupata taarifa zote wanazotaka. Huu ni wakati wa kusoma magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti kupitia e Gazeti,” amesema.

Baadhi ya wateja wa magazeti ya Mwananchi, Mwanaspoti na The Citizen, Mkoani Mbeya wamesema ni wakati sahihi kwa kampuni hizo kutumia teknolojia ya mawasiliano katika kuwafikishia huduma za mazageti.

“Ni mfuatiliaji mzuri wa taarifa zinazotolewa na Mwananchi, kila siku lazima nisome gazeti na kama nikikosa huwa naingia kwenye mitandao yao kwa hiyo uwepo wa application hiyo utasaidia, badala ya kufuata gazeti liliko nitakuwa napakua tu kwenye simu yangu,” amesema Festo Mwambeta, Mkazi wa Sowezi Jijini Mbeya na kuongeza;

“Ombi langu wawahi kutuletea, unajua Mbeya magazeti yanafika kumeshakucha kwa hiyo nataka niwe nasoma kabla sijaamka kitandani.”