Mdundo.com yatoa fursa ya kipekee kwa waumini wa dini ya Kiislamu

Muktasari:

Kampuni ya huduma za mziki mtandaoni ya Mdundo.com kwa mara ya kwanza katika msimu wa Ramadhani ulianza Aprili 1 hadi 30, imetoa fursa ya kipekee kwa waumini wa dini ya Kiislamu kusikiliza na kupakua mpangilio wa muziki maalum wa Kaswida kutoka kwa maDJ mbalimbali kukuza safari yao ya kiroho.

Kampuni ya huduma za mziki mtandaoni ya Mdundo.com kwa mara ya kwanza katika msimu wa Ramadhani ulianza Aprili 1 hadi 30, imetoa fursa ya kipekee kwa waumini wa dini ya Kiislamu kusikiliza na kupakua mpangilio wa muziki maalum wa Kaswida kutoka kwa maDJ mbalimbali kukuza safari yao ya kiroho.

Akitangaza fursa hiyo jijini Dar es Salaam jana Meneja Miradi wa kampuni hiyo,  Frida Muraguli amesema ofa hiyo ya kwanza na ya kipekee ipo wazi kwa waumini wa dini zote ikiwemo wapenzi wengine wote wa muziki.

Amesema fursa hiyo itawawezesha wateja kupata moja kwa moja muziki mchanganyiko kutoka kwa MaDJ maalum kwa bei nafuu ya sh.100, sh.500 au sh. 3,000 - kwa siku, wiki au mwezi kupitia Mdundo.com.

"Hii ni njia yetu ya kuwatakia ndugu zetu Waislamu Ramadhan Kareem – kwa kuwapa fursa ya kipekee ya kutiririsha, kusikiliza na kupakua muziki wa Kaswida na kupata maudhui mengine ya aina mbali mbali kwa gharama nafuu kupitia huduma yetu bora zaidi ya mziki mtandaoni - Mdundo.com," almesema Meneja Masoko wa kampuni hiyo Afrika Mashariki, William Abagi

Amesema maudhui husika yanajumuisha aina mbali mbali za muziki ikiwemo Kaswida, Taarab, Singeli, Injili, Bongo, Naija/Afrobeat, Amapiano, Hip hop na nyingine nyingi.

Katika fursa huyo, Clouds FM pia wameungana na Mdundo.com kuwapa wasikilizaji muziki mchanganyiko kutoka kwa MaDJ maarufu wa Clouds FM, ambao sasa unapatikana kupitia ukurasa wa mdundo.com/cloudsfm.

Amesisitiza kuwa ukuaji wa kasi wa huduma za kutiririsha na kupakua muziki mtandaoni kumeifanya Mdundo.com kuwekeza muda, jitihada na teknologia nyingi zaidi ili kuwainua wasanii wa kiTanzania.

"Mamilioni ya watumiaji wa mtandao kutoka ndani na nje ya nchi wanatumia huduma hiyo kusikiliza na kupakua muziki wa wasanii mbalimbali wa ndani na nje ya nchi.

"Vile vile, wasanii wengi wa Kitanzania wamechangamkia fursa hii mpya kwa kujisajili na kusambaza maudhui yao kwenye Mdundo.com ili kuwawezesha kuwafikia mamilioni ya wasikilizaji na mashabiki wanaotumia mtandao huu kila mwezi, " amesema
Imani na muziki zitaungana pamoja sasa kwenye Mdundo.com ili kukonga nafsi za waumini wote katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhan – baada ya kampuni hiyo maarufu ya kutiririsha mziki mtandaoni kuzindua ushirikiano huo wa kipekee na kampuni ya teknologia ya Vodacom pamoja na kituo cha redio Clouds FM.