Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Membe aagwa Dar

Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango akiaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe leo Mei 14, 2023 katika viwanja vya Karimjee. Picha na Michael Matemanga

Muktasari:

  • Maelfu ya maombolezaji wameshiriki kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.

Dar es Salaam. Viongozi mbalimbali wameshiriki kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, akiwemo rafiki yake, Jakaya Kikwete Rais wa awamu ya nne.

Membe alifariki dunia Mei 12, 2023 katika hospitali ya Hubert Kairuki jijini Dar es Salaam, alipokuwa anapatiwa matibabu baada ya kuugua ghafla.

Hafla ya kuaga mwili wake imefanyika katika viwanja vya Karimjee jijini hapa na iliongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Baada ya salamu za viongozi mbalimbali, mwili wa Mwanasiasa huyo ulianza kuagwa saa 7:30 akianza Rais Samia na kufuatiwa na Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango.

Aliyefuatia baada ya Dk Mpango ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kisha wakafuatia viongozi wengine na baadaye waombolezaji wengine.

Saa 8:00 mshereheshaji aliwaarifu waombolezaji kuwa Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete ametua nchini kutoka Korea na kwamba atawasili viwanjani hapo kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho.

Kikwete alisafiri kwenda nchini humo wiki chache zilizopita kwa ziara ya kikazi na kwamba taarifa ya kifo cha Membe zilitolewa akiwa huko.

Kwa muda mrefu Membe na Kikwete wamekuwa marafiki wa karibu, hatua iliyosababisha baadhi kuhusisha ukaribu huo unachagizwa na uhusiano wa kindugu.