Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Meya Iringa akemea wananchi kutupa taka za moto kwenye makontena

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada aliyevaa kaundasuki ya ugoro katikati akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kitaifa wa JATA.

Muktasari:

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa, Ibrahim Ngwada amesema Manispaa hiyo inakabiliwa na uchakavu wa makontena ya kuhifadhia taka kutokana na wananchi kutupa taka zenye moto katika kontena hizo.

Iringa. Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa, Ibrahim Ngwada amesema Manispaa hiyo inakabiliwa na uchakavu wa makontena ya kuhifadhia taka kutokana na wananchi kutupa taka zenye moto katika kontena hizo.

Ngwada amesema hayo wakati akifungua mkutano wa umoja wa Watanzania waliosoma nje ya nchi kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) na kubainisha kuwa endapo wananchi wataacha kutupa taka zisizohitajika katika kontena hizo watasaidia katika utunzaji wa vifaa hivyo.

"Manispaa inakabilia na changamoto ya magari machache ya kubebea taka hivyo tunaomba wananchi waache kutupa taka za moto kwenye makontena haya kwa sababu wanachangia kwa kiasi kikubwa uchakavu wa makontena, mkitupa taka zinazohitajika na sahii makontena yatakiwa salama na mioto haiwezi kuleta madhara pindi taka zinapokuwa zimekuwanywa sehemu" amesema

Amesema Halmashauri inampango wa kuendelea kuyakarabati kila yanapoharibika lakini wanaendelea kutoa elimu ya utunzaji wa usafi wa mazingira kuhakikisha mji wa Iringa unaendelea kuwa safi.

"Tunaishukuru JATA kwa kuendelea kuisaidia Manispaa ya Iringa katika utunzaji wa mazingira na usafi kwa kipindi kirefu Halmashauri ya Iringa imekuwa ikishika nafasi ya juu kwenye usafi wa mazingira, mwaka huu wa 2021 tumeshiriki na tunaamini tutashika nafasi ya kwanza" amesema

 Mwenyekiti wa JATA, Taifa Gregoly Mlay amesema kwa Mkoa wa Iringa umoja huo umejikita katika usimamizi wa taka kwa kuangalia taka hizo zinawezaje kutumika tena au kupunguzwa au kuzalisha kitu kingine kipya.

Mlay amesema kuwa wamekuwa wakisaidia vikundi kubuni kutumia chupa za vioo na plastiki kutengeneza mapambo ili kuendelea kuufanya Mkoa wa Iringa kuendelea kuwa safi zaidi.

"JATA inatoa elimu kwa vikundi na jamii kwa ujumla juu ya ukusanyaji taka na utupaji wa taka zilizo salama ili zisiweze kuleta madhara pindi zinapokuwa zimehifadhiwa kwenye vyombo vya kuhifadhia taka na kuviacha vikiwa salama" amesema.

Kwa upande wake Ofisa Afya ya Mazingira wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Christian Ndenga amesema suala la taka ngumu ni muhimu kushirikisha wadau ili waaweze kuzidhibiti kabla ya kuzipeleka dampo.

"Lazima kuwe na utenganishaji wa taka kabla ya taka kuhifadhiwa hivyo halmashauri inavikundi 18 ambavyo tunavifundisha kuviwezesha jinsi ya kuchakata takataka ili waweze kutengeneza mboji na wengine waweze kukusanya taka kama skrepa, lakini kumekuwa na changamoto kubwa katika utenganishwaji wa taka" amesema