Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Meya manispaa ya Moshi awataka waliovaa barakoa kuzivua

Meya manispaa ya Moshi awataka waliovaa barakoa kuzivua

Muktasari:

  • Juma Raibu Juma, meya wa manispaa ya Moshi amewataka wajumbe wa baraza la madiwani la manispaa hiyo kuvua barakoa kwa maelezo kuwa mji wa Moshi upo salama, agizo alilolitoa baada ya kuwasimamisha waliokuwa wamevaa barakoa hizo.

Moshi. Meya wa manispaa ya Moshi,  Juma Raibu Juma amewataka wajumbe waliovaa barakoa katika kikao cha baraza la madiwani kuzivua kwa madai kuwa manispaa hiyo ipo salama.

Ametoa agizo hilo leo Alhamisi Januari 28, 2021 wakati wa ufunguzi wa kikao cha bajeti cha baraza hilo baada ya kuwataka waliovaa barakoa kusimama na kisha kuwataka wavue.

"Kabla ya kufungua kikao chetu niwaombe wote waliovaa barakoa wasimame. Vueni barakoa zenu,  manispaa yetu ipo salama, mimi mstahiki meya sijavaa barakoa wewe uliyevaa ina maana unajipenda zaidi,” alihoji.

Meya manispaa ya Moshi awataka waliovaa barakoa kuzivua