Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Meya wa Moshi aagiza Sh3.2 milioni za kununua bastola ya mkurugenzi kurejeshwa

Meya wa Moshi aagiza Sh3.2 milioni za kununua bastola ya mkurugenzi kurejeshwa

Muktasari:

  • Meya wa manispaa ya Moshi, Juma Raibu ameagiza Sh3.2 milioni zilizotengwa na halmashauri ya manispaa hiyo kwa ajili ya kununua bastola ya mkurugenzi kurejeshwa.

Moshi. Meya wa manispaa ya Moshi, Juma Raibu ameagiza Sh3.2 milioni zilizotengwa na halmashauri ya manispaa hiyo kwa ajili ya kununua bastola ya mkurugenzi kurejeshwa.

Raibu ametoa tamko hilo leo Ijumaa Mei 28, 2021 katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ofisi za mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk Stephen Kagaigai ambaye pia alishiriki kikao hicho.

Amesema fedha hizo zilipitishwa na halmashauri hiyo mwaka 2015 na kubainisha kuwa ni matumizi mabaya ya fedha za umma.

"Kuna fedha zilipitishwa mwaka 2015 kiasi cha Sh3.2 milioni kwenye akaunti ya halmashauri kununua bastola ya mkurugenzi, haya  ni matumizi mabaya ya fedha za umma, nimeagiza fedha hizi zirudishwe mara moja," amesema Raibu.