Mfumo mpya kuingia stendi ya Magufuli walalamikiwa kuchelewesha abiria

Msongamano uliosababisha abiria kuchelewa umesababisha matumizi ya tiketi za kawaida kurejea katika Stendi ya mabasi ya Magufuli, mfumonhuo ulianza Jumatatu ya Februari 20,2023 lakini umekuwa ukilalamikiwa kutokana na kuwekwa kwenye geti moja tu jambo linalosababisha msongamano.

Muktasari:

  • Ikiwa ni siku ya pili kutumika kwa mfumo was N-Card katika kituo cha mabasi cha Magufuli, changamoto imeibuka ya ucheleweshaji wa abiria kuingia kituoni hapo, hali iliyolazimisha matumizi ya risiti za karatasi ili kuwawahisha abiria kwenye mabasi.

Dar es Salaam. Zikiwa zimepita siku mbili tangu tangu Manispaa ya Ubungo, ianze utaratibu mpya wa kuingia na kadi katika stendi ya mabasi ya Magufuli, mfumo huo umelalamikiwa kuchelewesha abiria, huku baadhi ya madereva nao wakilalamikia ucheleweshaji wa safari zao.

 Hatua ya matumizi ya N- Card yalianza Jumatatu Februari 20, 2023 ili kupunguza changamoto ya foleni hasa wakati asubuhi, ambapo kuna kuwa abiria na wasindikizaji wengi katika eneo hilo pamoja na kudhibiti upotevu wa mapato.

Mwananchi Digital ilifika kituoni hapo leo Februari 22 na kukuta abiria wakitumia tiketi za kawaida huku wakilalamika baadhi ya milango kuchelewa kufunguka na kusababisha foleni.

Mariam Jumbe abiria aliyekuwa anasafiri kwenda Tanga amesema baada ya kupewa kadi kila akiweka kwenye mashine geti limekuwa halifunguki, Jambo linalosababisha msongamano.

 "Pale unavyoona kuna milango zaidi ya mitatu, ila  kuna wakati unakuta mlango mmoja au miwili inafanya kazi Jambo linalisababisha msongamano, isitoshe asubuhi tunakuwa tunawahi magari na abiria ni wengi," amesema Mariam.

Mmoja wa madereva alliyejitambulisha kwa jina la Ahmed Issa alisema mfumo huo unachelewesha magari kutoka kwani aabirianwamekuwa wakiingia taratibu licha ya wengi wao kuwa na tiketi.

"Huu mfumo hawajipanga ukiangalia madirisha yakutolea kadi yako kumi na mfumo huu imefungwa kwenye geti moja licha yakuwepo mageti zaidi ya matatu kwanidadi ya abiria wanapoingia hapa sio wakitumia geti moja," alisema Issa.

Dereva mwingine ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema, mfumo huo unasababisha magari kuchelewa kutoka kwani unasababisha abiria kushindwa kuingia kwa muda kutokana na mashine hizo kuchukua muda kuruhusu mtu kuingia.

Kwa upande wa mawakala waliokuwa wanalalamikia mfumo huo kutokana na kuwafanya kulipa kila wanapokuwa wanaingi wameiomba Serikali kusitisha kwanza utaratibu huo Hadi pale watakapojipanga kwani unasababisha adha kwa abiria hasa nyakati zanasubuhi.

"Unakuta gari unaondoka saa 12 halafua abiria anakuwa getini saa 12 kasoro unategemea nini kama sio kuachwa, tunaomba utaratibu huu usitishwe hadi pale mashine zitakapofungwa kwenye kila geti," amesema Rogers

Mfumo huo uliofungwa kwenye geti moja kati ya matano ya kuingilia kwenye stendi hiyo, kuna madirisha kumi ya kununulia kadi hukunkukiwa na milango saba ya kuingilia ndani jambo linalosababisha msongamano.

Jitihana za kuupata uongozi wa Manispaa ya ubungo na meneja wa stendi hiyo bado zinaendelea.