Mghwira aagwa Arusha

Mghwira aagwa Arusha

Muktasari:

  • Shughuli za kuendelea kumuaga aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira zinaendelea nyumbani kwake Manyata Jijini Arusha huku tahadhari za ugonjwa wa corona zikiendelea kuchukuliwa.

Arusha. Shughuli za kuendelea kumuaga aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira zinaendelea nyumbani kwake Manyata Jijini Arusha huku tahadhari za ugonjwa wa corona zikiendelea kuchukuliwa.


Mghwira alifariki dunia mchana wa Julai 22, 2021 wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru iliyopo jijini Arusha.


Wakuu wa mikoa ambao wamefika mpaka sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Adam Malima pamoja na wakuu wa  wilaya za  mkoa wa Kilimanjaro.


Salamu za rambirambi zinaendelea kutolewa hapa nyumbani kwake Manyata na kisha baadaye mwili wake utaondolewa nyumbani hapa na kupelekwa nyumba yake nyingine iliyopo Makumira kwa ajili ya maziko.


Mghwira ameacha watoto wa kiume watatu.