Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mgogoro wa mgawano wa fedha za Tasaf kati ya mama na mwanaye wasuluhishwa

Mkazi wa kijiji Runazi kata Runazi, Anastazia akiwasilisha lalamiko lake la watoto wake kunyimwa fedha za mpango wa Tasaf na bibi yao kwa Timu ya kampeni ya  msaada wa Kisheria ya Mama Samia.

Biharamulo.Timu ya Kampeni ya Msaada wa kisheria ya Mama Samia katika Halmashauri ya wilaya Biharamulo imefanikiwa kumaliza Mgogoro kati ya Mama na Mwanaye waliokuwa wakigombania Fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tasaf.

Mkazi wa kijiji na kata Runazi Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera, Anastazia Mathias (35), amefikisha malalamiko la mama mzazi, Astelia Mathias (65) kuwanyima gawio la fedha za mpango wa kusaidia kaya masikini nchini TASAF wajukuu zake watatu ambao alikuwa akiishi nao kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo.

Anastazia, alifikisha lalamiko kuhusu  watoto wake watatu kunyimwa haki ya kupata mgawanyo wa kiasi cha fedha Sh12,000 kutoka kwa bibi yao ambaye ni  Astelia (65) ambacho alistahili kuwapatia kwa ajili ya matumizi baada ya kupokea Sh24,000 kila mwezi kwa ajili ya kusaidia matumizi kutoka mpango wa Tasaf.

Anastazia amesema kutokana na ugumu wa maisha baada ya kumpoteza mzazi mwezie baba wa watoto wake watatu ambao hakuwataja majina aliamua kuwapeleka watoto wakaishi na mama yake (Bibi) yeye akaanza kutafuta vibarua vya kufanya"kulima" katika wilaya nyingine mbali mbali jambo ambalo halikuwa rahisi na baadae kamati ya kijiji katika mpango wa kitaifa wa kusaidia kaya masikini ukachukua uamzi wa kusaidia familia hiyo.

Anastazi amesimulia kisa cha kufikisha lalamiko lake nikutokana na mama yake kupokea fedha zote kwenye namba yake ya simu kama alivyoelekezwa na baada ya hapo afanye gawio kwa wajukuu zake  kwa ajili ya kununua unifomu na matumizi mengine ila yeye hakufanya hivyo mpaka akalazimika kurudi nyumbani hali ikiwa mbaya kwa watoto wake.

"Alikuwa akipokea fedha kama kawaida kila mwezi Sh24,000 kiasi cha Sh12,000 ni kwa ajili ya wanangu  ila mama hakufanya hivyo nilipojaribu kumshauri alikuwa akinitukana sana"amesema

Mwenyekiti wa kijiji Runazi, Innocent Gendalikoma aliyeungana na timu ya msaada wa kisheria kusuruhisha mgogoro huo, awali amesema jambo hilo limewahi kufikishwa kwenye kamati ya kijiji ya mpango wa kusaidia kaya masikini Tasaf wakasuluhisha mgogoro huo ila bibi huyo hakuonyesha kuridhika.

"Nadhani leo wote mtusaidie kupata suluhu ya familia hii kuhusu fedha hizi hawa tuliwapatanisha lakini hawakuwahi kuridhika na mgogoro ni wa muda mrefu sana zaidi ya mwaka mwafaka umekosa bibi kwa sasa amebaki na mjukuu mmoja"amesema Innocent

Naye, Mkazi wa kijiji hicho cha Runazi Astelia Mathias (65) mlalamikiwa wakati anawasilisha mchango wake kuhusu malalamiko hayo yaliyomkabili ameonesha kukiri kutowapatia haki wajukuu zake akidai fedha alikuwa akizitumia kwenye mahitaji mengine kulingana na uhitaji wa familia.

Timu ya Kampeni msaada wa kisheria ya Mama Samia ikiongozwa na mratibu Mkuu, Salome Mwakalonge pamoja na msajili msaidizi, Darra Siras wamefanikiwa kusuluhisha mgogoro huo baada ya kuwakutanisha wote kwa pamoja mama na mwaye na kushauri Astelia ambaye ndiye mpokeaji mkuu wa fedha ahakikishe anafanya mgawanyo wa fedha kama alivyoelekezwa.

Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia iliyofanyika katika Mkoa wa Kagera na wilaya Biharamulo kuanzia Aprili 15, 2025 na iliyotarajiwa kukamilika Aprili, 24, 2025 imeongezewa siku tano kwa ajili ya kuendelea kuwasikiliza wananchi na kutatua migogoro yao.