Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Miradi kibao ya maji Buchosa yakwama

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Injinia Gerson Lwenge

Muktasari:

Hayo yamebainika baada ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Zainab Terack kutembelea miradi hiyo na kujionea jinsi wananchi wanavyoteseka kupata huduma hiyo.

Sengerema. Miradi ya Maji ya Lumeya, Kalebezo, Nyehunge na Nyakaliro-Bukokwa wilayani hapa Mkoa wa Mwanza, imekwama licha ya kutakiwa kukamilika baada ya miezi sita tangu ilipoanza kujengwa mwaka 2012.

 Hayo yamebainika baada ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Zainab Terack kutembelea miradi hiyo na kujionea jinsi wananchi wanavyoteseka kupata huduma hiyo.

 Terack ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, alisema baada ya kuunda kamati ya uchunguzi, ilimpatia ripoti iliyobainisha kuwapo uzembe na madudu katika miradi hiyo inayotekelezwa na kampuni za Pet Cooperation Ltd na Luneco Investment.

 ‘’Naomba mamlaka husika ziwarejeshe aliyekuwa mhandisi wa Halmashauri ya Sengerema na Mkurugenzi wake wa mwaka 2012, waje kujibu tuhuma za kulipa makandarasi fedha nyingi wakati kazi haikufanyika,” alisema.