Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Misaada ya washirika yapungua Tanzania kwa asilimia 39.1

Muktasari:

  • Serikali inatarajia kukusanya na kutumia Sh62.33 trilioni, ikiwa ni ongezeko la asilimia 10.3 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2025/26. 132.

Dar es Salaam. Misaada ya washirika wa maendeleo Tanzania inatarajiwa kupungua kwa asilimia 39.1 kwa mwaka 2026/27 ikilinganishwa na fedha zilizoahidiwa mwaka 2025/26.

Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omari ameeleza hayo leo Alhamisi, Juni 11, 2026 wakati akiwasilisha Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2026/27 ya Sh62.3 trilioni, bungeni jijini Dodoma.

“Hali hii inatokana na kubadilika kwa sera za baadhi ya washirika wa 155 wa maendeleo. Tunawashukuru washirika wetu wa maendeleo kwa msaada wao pale walipoweza,” amesema.

Hata hivyo, Balozi Omar amesema Tanzania ni Taifa na wananchi wake ndio wenye wajibu wa kulijenga.

Amesema ni wajibu wa wananchi wote kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi, kulipa kodi kwa hiari, na kushikamana na Serikali katika kuleta maendeleo.

Amesema mwaka 2026/27 Serikali inatarajia kukusanya na kutumia S 62.33 trilioni, ikiwa ni ongezeko la asilimia 10.3 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2025/26. 132.

Waziri huyo amesema mapato yanatarajiwa kuwa Sh46.79 trilioni ambapo mapato ya kodi ni Sh36.99 trilioni, mapato mengine ni Sh9.24 trilioni ikijumuisha mapato ya mamlaka za serikali za mitaa Sh1.97 trilioni na misaada kutoka kwa washirika wa maendeleo Sh 563.1bilioni.

“Ili kuendana na dhamira yetu ya kujitegemea katika uendeshaji wa Serikali na maendeleo, takribani robo tatu ya bajeti yote ya mwaka 2026/27, sawa na asilimia 74.2 inatarajiwa kugharamiwa na mapato ya ndani,” amesema.