Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Miti 7,000 yapandwa kulinda vyanzo vya maji Mbarali

Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Reuben Mfune akishiriki upandaji miti katika eneo la kudakio cha maji cha usangu kilichopo katika kijiji cha Lugelele Wilayani Mbalali kwa lengo la kuhifadhi vyanzo vya maji kwa kupanda miti rafiki na maji kupitia mradi wa REGROW kwa kushirikiana na bodi ya maji bonde la Rufiji.

Muktasari:

Bodi ya Maji Bonde la Rufiji kwa kushirikiana na halmashauri ya Wilaya ya Mbarali imezindua mpango wa upandaji miti rafiki kwenye vyanzo vya maji vinavyotiririsha maji yake kwenye mto Ruaha mkuu kwa lengo la kurejesha mtiririko wa maji kwenye mto huo.

Mbarali. Bodi ya Maji Bonde la Rufiji kwa kushirikiana na halmashauri ya Wilaya ya Mbarali imezindua mpango wa upandaji miti rafiki kwenye vyanzo vya maji vinavyotiririsha maji yake kwenye mto Ruaha mkuu kwa lengo la kurejesha mtiririko wa maji kwenye mto huo.

Mpango huo ulizinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Reuben Mfune na kuwaelekeza wakala wa huduma za misitu Tanzania TFS kuhakikisha wananchi wote wanaokata miti na kuisafirisha kwa baiskeli na pikipiki au mkaa na kuni  wadhibitiwe ili kuendelea kutunza vyanzo vya maji.

Mfune ametoa maelekezo hayo wakati wa uzinduzi wa zoezi la upandaji miti katika wilaya hiyo kwa kushirikia na bodi ya bonde la mto Rufiji chini ya mradi wa REGROW ambapo miti 7,000 ilipandwa katika kidakio cha Usangu kilichopo Kijiji cha Lugelele.

Mfune amesema pamoja na kazi hiyo ya upandaji miti ni vyema kama watu wanaokata miti na kusababisha uharibufu wa mazingira wachukuliwe hatua za kisheria ili zoezi hilo la upandaji miti liweze kuzaa matunda.

“Mimi nisingependa kuendelea kuwaona wananchi wakiendelea kukata miti kwa sababu hatuwezi kuwa tunafanya kazi ya kupanda miti wengine wanakata miti,naomba nitoe maelekezo kwa TFS wale ambao bado wanaendelea kukata miti na kuisafirisha kwa kutumia pikipiki na baiskeli hili sio jambo jema hatuwezi kuwa tunapanda miti wengine wanendelea kukata kwa kasi kubwa naomba muwachukulie hatua kali”

Amesema wale ambao wanavibali wana ruksa ya kuendelea kufanya hivyo kwa sababu wanapewa eneo maalum kwa ajili ya kukata ili miche mingine iendelee kuota Zaidi ila wale wanaofanya uharibifu tuwadhibiti.

“Niwaombe bonde la Rufiji kazi ya upandaji miti iwe endelevu sehemu ya mbarali bado uhalibifu upon a bado kwa hali ya kawaida tunahitaji miti mingi ili kuhifadhi hii mito inayorisha mito mikubwa ambayo ni manufaa kwa nchi”.

Kwa upande wake msimamizi wa mradi wa REGROW upande wa bodi ya maji bonde la Rufiji David Mginya amesema lengo kuu ni kuboresha na kusimamia vyanzo vya maji ambavyo ni vyanzo vya mto Ruaha mkuu na kuongeza mtiririko wa maji.

Amesema hifadhi ya Taifa ya Ruaha inategemea mto Ruaha kwa maana ya wanyamapori kuweza kustawi kwa kuchochea shughuli za kitalii pia mto huo unategemewa katika shughuli za uzalishaji wa umeme kwenye bwawa la mtera.

“Kupitia mradi huu wa REGROW tunakazi ya kusimamia maeneo ya vyanzo vya maji kwa kupanda miti,kuimarisha mifumo ya ufatiliaji wa matumizi ya maji na kuimarisha taasisi za usimamizi wa rasilimali za maji na Shughuli za upandaji miti kwa kuhakikisha maeneo ya vidaka maji yana miti ya kutosha miti rafiki na maji ambayo inatunza maji”.

Abisai Chilunda Ofisa wa maji kidakio cha Ruaha Mkuu amesema kupitia mradi wa REGROW kwenye upande wa bodi yam aji bonde la Rufijii wamehakikisha maji yanatiririka bila shida yeyote kwa kusimamia mtiriliko huo pamoja na kutoa elimu kwa wananchi.

“Kwa mujibu wa sheria mtumia maji anapopewa kibali cha kutumia maji huwa wanaainisha kiasi cha maji anachopaswa kutumia,hivyo tumefanikiwa kudhibiti  watu wanaotumia maji bila kuwa na vibali na wale wanaotumia zaidi ya kiasi cha maji ambacho kipo ndani ya vibali vyao”

Aidha wanafunzi wa shule ya sekondali na msingi kutoka katika Kijiji hicho cha Lugelele walishiriki kupanda miti katika eneo la kidakio cha Usangu ili waweze kujifunza namna ya utunzaji wa vyanzo vya maji na mazingira kwa ujumla kutokana na wananchi wengi kushindwa kupata elimu hiyo.

Kwa miaka miwili mfurulizo mto mkuu ruaha umekuwa ukitiririsha maji bila kukauka jambo ambalo limesaidia wanyama kupata maji hifadhini kupitia mto huo na kuondoka na adha ya wanyama kutoka nje ya hifadhi kutafuta maji na kusababisha wanyama kuuawa na kuvamia makazi ya wananchi.