Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mjamzito adaiwa kubakwa hadi kufa Iringa


Muktasari:

  • Jeshi la Polisi mkoani Iringa linamshikilia mkazi wa Manispaa, Mohamed Njali, kwa tuhuma za kumdhalilisha kijinsia mama mjamzito, Atka Kivenule na kumsababishia kifo chake.

Iringa. Jeshi la Polisi mkoani Iringa linamshikilia mkazi wa Manispaa, Mohamed Njali, kwa tuhuma za kumdhalilisha kijinsia mama mjamzito, Atka Kivenule na kumsababishia kifo chake.

Tukio hilo limetokea Jumamosi usiku mtaa wa Maweni, kata ya Kitazini/Myomboni ambapo mtuhumiwa huyo alivamia nyumbani kwa Adeline Kileo, saa 5 usiku.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Allan Bukumbi, alikiri kutokea kwa tukio hilo na wanaendelea na uchunguzi ili kujua sababu za mauaji hayo.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa, Alfred Mwakalebela amethibitisha kupokea mwili wa mwanamke anayedaiwa kubakwa hadi kufariki akiwa na ujauzito wa wiki 10.
“Inasemekana alikuwa amelala ndani akavamiwa na mtu na katika uchunguzi tumegundua alivunjwa koromeo tulikuta michubuko inaonekana mbakaji alikuwa akimnyonga shingo ili atimize azma yake,’ alisema Mwakalebela.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi amethibitisha kutokea tukio hilo na kwamba, uchunguzi zaidi unaendelea.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Mohamed Moyo alisema mtuhumiwa amekamatwa na kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi kwa hatua zaidi.

Moyo alisema hajafurahishwa na matukio ya ukatili yanayoendelea mkoani hapo na kusema inahitajika nguvu ya pamoja kati ya Serikali, wananchi na wadau mbalimbali katika kupiga vita matendo hayo ya udhalilishaji wa kijinsia.

“Tunawaomba viongozi wa dini waendelee kuzungumza na waumini wao, kubwa zaidi wajue kumtanguliza Mungu, wabunge wawe na ajenda ya kudumu ya kukemea masuala ya udhalilishaji, ubakaji, mauaji na kuondokana na imani za kishirikina kwamba wakibaka au kuua watapata utajiri,” alisema Moyo.

Kwa upande wake, Balozi wa mtaa wa Maweni, Yasin Kisogwe alisema aliletewa taarifa hizo za kusikitisha kuwa amevamiwa katika nyumba yake na mkewe kubakwa hadi kufa.

“Kwa kushirikiana na jeshi la polisi, tulikwenda nyumba ya mtuhumiwa na alikamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi na kuanza kufanya upekuzi nyumbani kwake na ilipatikana simu ya marehemu,” alisema.

Akizungumza kwa majonzi, mume wa marehemu, Adeline Kileo alisema siku ya tukio mke wake alitoka kazini kutokana na hali yake ya ujauzito alimuomba mumewe amsaidie kupika.

Alisema baada ya kumaliza kula yeye na kaka yake walirudi dukani kuendelea na biashara kisha wakaenda kuangalia “pambano la ngumi la Mandonga.”

Alisema wakiwa katika mgahawa wanaangalia pambano mtuhumiwa alimfuata na kumwambia “mkeo ni mzuri sana, jirani ana shepu hatari.”

Kileo alisema, baada ya kusikia anazungumza maneno hayo, “sikuyapenda nikampoteza na kuendelea kuangalia ngumi mimi na wenzangu.”

Alisema, baada ya kutoka kuangalia pambano la ngumi, alishangaa kukuta milango ya nyumba yake ipo wazi na kuingia ndani hakuamini macho yake alipomwona mkewe akiwa amelala kitandani kifudifudi akiwa uchi wa mnyama.

“Nikamuita mtoto hakuitika, sikumpata sehemu yeyote, ndipo tukaamua kumchukua mke wangu kumpeleka hospitali ya jirani ambapo tuliambiwa ameshafariki” alisema.

“Alikuwa ni mjamzito wa miezi miwili, naliomba Jeshi la Polisi litusaidie kupata haki na kutoa adhabu kali kwa watuhumiwa wa matukio haya ili yasiendelee kwa familia nyingine au watu wengine kufanyiwa,” alisema.