Mji wazizima mapokezi mwili wa Askofu Mwanisongole

Baadhi ya waombolezaji katika ibada ya mazishi ya Askofu Mkuu Mstaafu wa Tanzania Assembles of God (TAG) Dk Ranwell Mwanisongole katika viwanja vya CCM Vwawa mkoani Songwe. Picha na Stephano Simbeye
Muktasari:
Mji Mdogo wa Vwawa leo Desemba 30, 2021 umezizima ukiupokea mwili wa aliyekuwa Askofu Mkuu Mstaafu wa Tanzania Assembles of God (TAG), Dk Ranwell Mwanisongole baada kuwasili ukitokea jijini Dar es Salaam.
Songwe: Mji Mdogo wa Vwawa leo Desemba 30, 2021 umezizima ukiupokea mwili wa Askofu Mkuu Mstaafu wa Tanzania Assembles of God (TAG), Dk Ranwell Mwanisongole baada kuwasili ukitokea jijini Dar es Salaam.
Umati wa watu umeonekana kuanzia mitaa ya Ichenjezya iliko nyumba yake lakini wakielekezwa kwenda Uwanja wa CCM Vwawa ambako ibada ya mazishi ikinaendelea.
Mbali ya wananchi wa kawaida waliofurika katika uwanja huo, wapo viongozi mbalimbali wa kisiasa na kidini wameshiriki ibada hiyo.
Miongoni mwa viongozi hao ni Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dk Tulia Ackison, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Omary Mgumba, Jaji Mahakama Kuu Ole Gabriel na Mbunge wa Vwawa, Dk Japhet Hasunga.
Ibada hiyo ya mazishi ya kitaifa imeongozwa na Askofu Mkuu wa TAG, Barnabas Mtokambali.
Profesa Mwanisongole alifariki dunia Jumamosi Desemba 25, 2021 katika hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam.