Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mkalimani akwamisha kesi wanaodaiwa kuingia tani 11 dawa za kulevya

Washtakiwa saba wanaokabiliwa na kesi ya kuingiza nchini sampuli za dawa za kulevya aina ya Mitragyna speciosa zenye uzito wa kilo 11,596, wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Picha na Hadija Jumanne.

Muktasari:

  • Shaweji na wenzake wanadaiwa kuingiza nchini shehena hiyo ya dawa za kulevya aina ya  Mitragyna Speciosa zenye uzito wa kilo 11,596.

Dar es Salaam. Upande wa Jamhuri katika kesi ya kuingiza nchini sampuli za dawa kulevya aina ya Mitragyna Speciosa zenye uzito wa kilo 11596, inayowakabili washtakiwa saba wakiwemo raia wa Sri Lanka, imeshindwa kuwasomea maelezo ya mashahidi na vielelezo kutokana na kukosekana kwa mkalimani anayetafsiri lugha ya Sri Lanka.

Dawa hizo zina madhara sawa na dawa za kulevya aina ya heroini, kokeini na Methamphetamine na moja kati ya madhara kwa watumiaji wa dawa hizo ni kupoteza kumbukumbu.

Mawakili wawili wa Serikali Mwandamizi, Frank Chanila na Tike Mwaisaka, wameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kuwa kesi hiyo imeitwa kwa ajili ya washtakiwa kusomewa maelezo yao, baada ya upelelezi kukamilika.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni Riziki Shaweji(40)mfanyabiashara na mkazi wa Masaki; Andrew Nyembe (34) wakala wa forodha;  Mariam Ngatila(40) mfanyabiashara na mkazi wa Masaki na Ramadhani Said(57) mfanyabiashara na mkazi wa Kifuru.

Wengine ni dereva, Godwin Mafikiri(40)mkazi wa Oysterbay pamoja na wafanyabiashara wawili raia wa Sri Lanka, Jagath Wellalage(46)mkazi wa Kinondoni na Santhush Hewage(25) mkazi wa Masaki.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 19066 la mwaka 2025.

Chanila amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Beda Nyaki anayesikiliza kesi hiyo kuwa,

"mheshimiwa hakimu, kutokana baadhi ya washtakiwa kutojua lugha ya Kiswahili na Kiingereza na kwa kuwa wamedai kuwa wanajua lugha ya nchi yao, ni vizuri tukatafuta mkalimani," ameshauri Chanila.

"Ni vyema mahakama ikahirisha  ili mkalimani atafutwe ndipo tuweze kuendelea na kesi hii, kwa muktadha huo tunaomba ahirisho fupi," amesema.

Kwa upande wa mawakili wanaowatetea washtakiwa hao, Michael Lugina, Philip Ilungu-, Nehemia Nkoko na Nazario Michael walikubaliana na ombi la upande wa Jamhuri la kuahirisha kesi hiyo kwa muda mfupi ili apatikane mkalimani.

Hakimu Beda baada ya kusikiliza maelezo ya a pande zote mbili, aliahirisha kesi hadi Mei 25, 2026.

Hata hivyo, washtakiwa wote wamerudishwa rumande kutokana kesi inayowakabili haina dhamana kwa mujibu wa sheria.

Katika kesi ya msingi, washtakiwa wanadaiwa Julai Mosi, 2025 katika Bandari Kavu ya Said Salim Bakhresa( SSB- ICD) iliyopo eneo la Sokota wilaya ya Temeke, washtakiwa kwa pamoja waliingiza sampuli zenye uhusiano na dawa za kulevya aina ya Mitragyna Speciosa zenye uzito wa kilo 11596, sawa na tani 11.5.

Washtakiwa hao wanadaiwa kuingiza dawa hizo katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kinyume cha sheria.

Kwa mara ya kwanza, washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo, Agosti 5, 2025 na kusomewa kesi ya uhujumu uchumi.