Mke wa bilionea Msuya: Nilipigwa na kitu kizito miguu

Muktasari:

  • Nilipigwa kwa muda mrefu sana kisha afande Ratifa aliniamuru ninyanyuke na nilipelekwa kwenye chumba kingine nililetewa chipsi na kuku lakini nilishindwa kula kutokana na maumivu makali niliyoyapata," amedai Miriam.

Dar es Salaam. Miriam Mrita, mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya, ameieleza Mahakama Kuu  kuwa alilazwa chini na kuanza kupigwa na kitu kizito kwenye miguu huku akiwa amefungwa kitambaa usoni sambamba na mikono yake kufungwa pingu.

Mbali na Miriam mshtakiwa mwingine ni mfanyabiashara Rebocatius Muyella ambao wanadaiwa kumuua kwa makusudi Aneth Msuya, dada wa marehemu bilionea Msuya.

Shauri hilo ambalo limeletwa kwa ajili ya kusikiliza utetezi mbele ya Jaji Edwin Kakolaki, upande wa jopo la mawakili wa serikali umeongozwa na Paul Kimweri, Yansita Peter na Generosa Montana.

Mshtakiwa huyo ameeleza hayo huku akiongozwa na Peter Kibatara  ambaye ndiye wakili wake, Mariam amedai kuwa kuwa Agosti 5, 2016 alipakizwa kwenye gari la polisi akitokea kituo cha Polisi cha Kati kilichopo Arusha, kuelekea jijini Dar es Salaam huku akiwa na askari polisi Davide Mahalaya, Jumanne Malangai na Ratifa Chiko.

Amedai kuwa wakati wakielekea jijini humo, walipofika eneo la Tegeta walisimamisha gari hilo ndipo afande Davide alimpa ishara Ratifa ambaye alimuamrisha mshtakiwa huyo ageuke na alianza kumfunga kitambaa usoni.

Baada ya kufungwa kitambaa hicho safari ilianza tena na walipofika kwenye kituo cha Polisi asichokijua alishushwa kwenye gari hilo huku akiwa ameshikwa mkono na afande Ratifa ambaye alimpeleka kwenye chumba kidogo kilichokuwa na nondo.

"Nilifunguliwa kitambaa usoni wakati nimeingizwa kwenye chumba hicho, sikuwahi kujua hadi leo ni kituo gani nilipelekwa wakati huo ilikuwa siku ya pili tangu nikamatwe Agosti 6, 2023," amedai mshtakiwa huyo.

Miriam aliendelea kusema kuwa baadaye alihamishwa kwenda chumba kingine wakati huo alifungwa kitambaa usoni alipelekwa kwenye chumba kidogo ambacho pembeni kilijengewa zege kwa ajili ya kunta

Miriam alidai walimfungua kitambaa hicho usoni huku afande Davide akimuuliza kwa nini amemuua Aneth alipokataa kuwa yeye hausiki ndipo Ratifa akamshika rasta alizokuwa amesuka alimvuta kwa nguvu.


"Muda wote huo sikupewa chakula tangu nilipokamatwa ndipo afande Ratifa alinifungua kitambaa na kunirudisha kwenye chumba cha awali chenye nondo alipoendelea kunihoji na nilimkatalia kuwa sijausika kumuua Aneth,” amesema na kuongeza;

“...ndipo alinifunga kitamba usoni na mikono yangu aliifunga nyuma kwa pingu na kuniacha nikiwa nimesimama pale yeye akatoka nje."

Amedai kuwa alipojaribu kumuuliza afande huyo iwapo atahitaji kusijadia atafanyaje, ndipo alipojibiwa kuwa hayo yalikuwa malipo ya mtu muuaji ambaye anatakiwa kukaa hivyo hadi Agosti 7, 2016.

Ameeleza kuwa kuwa Agosti 7, 2016 asubuhi, afande Davide, Jumanne na Ratifa walifika kwenye chumba hicho na kumuamuru mshtakiwa huyo awafuate walipo ndipo alisota hadi kwenye mlango wa geti walimfungua pingu na kitambaa alichofungwa machoni.

Baadaye aliamrishwa anyanyuke walimpeleka kwenye chumba ambacho kilikuwa na meza na viti vitatu ambapo alipelewa chai na maandazi mawili.

Alipomaliza kunywa chai hiyo alifungwa kitambaa usoni pamoja na pingu akarudishwa kwenye chumba cha awali ndipo afande Davide alimuuliza mshtakiwa huyo kama ana tatizo la kiafya.

Mshtakiwa huyo alimjibu alifanyiwa upasuaji wakati anajifungua ndipo alimuamlisha afande Ratifa amkague wakati huo Davide akiwa amekaa pembeni.

Anaeleza afande Ratifa alimuamlisha alale chali alibaini mshono ulikuwepo wakati akiwa amelala wakanyanyua miguu yote miwili na kuanza kumpigia na kitu kizito huku wakimuuliza kwa nini amemuua Aneth

"Nilipigwa kwa muda mrefu sana kisha afande Ratifa aliniamuru ninyanyuke na nilipelekwa kwenye chumba kingine nililetewa chipsi na kuku lakini nilishindwa kula kutokana na maumivu makali," amedai Miriam.

Anadai hayo yote yanaendelea hakuwahi kuruhusiwa kupiga mswaki, kuoga na kubadilisha nguo ndipo Agosti 8, 20216 alitolewa katika kituo hicho na kupeleka maeneo ya uwanja wa ndege wa Julius Nyerere katika kituo cha polisi alikaa ndani hadi Agosti 23, 2016 alipofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Shauri hilo limeahirishwa hadi Oktoba 25,2023 Kwa ajili ya kuendelea na utetezi