Mke wa Profesa Jay aeleza hali ya mumewe

Friday June 10 2022
By Nasra Abdallah

Dar es Salaam. Siku moja baada msanii Joseph Haule 'Profesa Jay' kuruhusiwa kutoka hospitali, mke wake ameeleza hali aliyonayo mumewe kwa sasa.

Profesa Jay ambaye aliwahi pia kuwa Mbunge wa Mikumi, alikuwa amelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa siku 127 na kuruhusiwa kutoka hapo jana.

Leo Ijumaa Juni 10 familia yake ikiongozwa na mdogo wake Nicholous Haule 'Black Rhino' na mke wake Grace Mgonjo wamesema wameona ni vizuri kujitokeza kutoa shukurani zao kwa kuwa Watanzania wamekuwa nao pamoja katika kipindi chote hiko kigumu na kueleza hali aliyo nayo kwa sasa.

Akizunguzia kuhusu hali yake ilivyo sasa baada ya kuruhusiwa, mke wa Profesa Jay, Grace Mgonjo, amesema msanii huyo ana hali nzuri kwani anaweza kuzungumza na kumkumbuka kila kitu.

"Kwa kweli tunamshukuru Mungu mume wangu anaendelea vizuri kwani hakuna aliyemsahau na pia anazungumza na kukumbuka kila kitu kama alivyokuwa awali huku akitaja baadhi ya watu ambao kawamiss na kutamani kuwaona,"amesema Grace.

Hata hivyo amesema ambacho bado kinamsumbua ni mwili kukosa nguvu lakini madaktari wamewaambia atapona taratibu huku wakimkazania vyakula na mazoezi madogo kama walivyoshauriwa hospitali.

Advertisement

"Tunashukuru anaongea ila viungo tu ndio bado havina nguvu na hii yote ni kutokanana kulala kitandani muda mrefu lakini tunaamini atapona taratibu kama madaktari walivyotuamvia kikubwa tunaomba watanzania mzidi kumuombea ili anyanyuke tena na kuendelea kuwaburudisha.

Advertisement