Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mkurugenzi FOA Motors akamatwa akidaiwa kutapeli

Muktasari:

  • Mkurugenzi kampuni ya Foa Motors amekamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Iringa kwa tuhuma za kutapeli Sh150 milioni kwa ahadi za kuwaagizia magari wateja wake.

  

Iringa. Jeshi la Polisi Mkoani Iringa linamshikilia  Michael Mbata (34),  Mkurugenzi wa Kampuni ya Foa Motors  kwa tuhuma ya kujipatia Sh150 milioni  kwa njia ya udanganyifu kwa wakazi wawili wa Mkoa wa Iringa kwa ahadi ya kuwaagizia magari kupitia kupitia kampuni hiyo.

Akizungumza na wanahabari leo, Septemba 20,2022 Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi, amesema mtuhumiwa huyo ambaye ni mkazi wa Dar es Salaam, alijipatia kiasi hicho cha fedha kutoka kwa Abdallah Huwel na Isaya Edward, wote wakazi wa Iringa.


Bukumbi amesema kuwa Abdallah Huwel alitoa Sh100 milioni kwa ahadi ya kuagiziwa gari aina ya Howo na Edward naye alitapeliwa Sh50 milioni kwa ahadi ya kununuliwa aina hiyo hiyo ya gari.

“Mtuhumiwa huyo aliwatapeli watu hao kwa ahadi ya kuwaagizia magari hayo kutoka Japan na Uingereza kupitia kampuni yake ya FOA Motors iliyopo Dar es Salaam.

“Pia alijipatia fedha kwa njia hiyo kutoka kwa watu mbalimbali kwa ahadi ya kuwaagizia magari kutoka nje ya nchi,” amesema.

Kamanda Bukumbi, amesema baada ya kupatiwa fedha hizo mtuhumiwa huyo alipoteza mawasiliano na watu hao kabla ya Agosti 20 mwaka huu kukamatwa akiwa katika eneo la Chanika jijini Dar es Salaam na kuletwa Iringa waliko walalamikaji hao.

 “Baada ya kukamatwa na kufanyiwa upekuzi nyumbani kwake alikutwa na magari mawili ambayo ni Nissan Dualis namba T 104 DZL lenye thamani ya Sh24 milioni na Subaru Impreza namba T 328 DZR lenye thamani ya Sh18 milioni,” amesema.

Amesema jeshi lake limekamilisha upelelezi na wakati wowote kuanzia sasa mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani.