Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mkurugenzi Jatu asubiri kupangiwa tarehe ya vikao

 Mkurugenzi JATU PLC, Peter Gasaya, akiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya kusomewa masharti ya dhamana. Hata hivyo mshtakiwa huyo ameshindwa kutimiza masharti hayo na hivyo kurudishwa rumande. Picha  na Hadija Jumanne

Muktasari:

  • Gasaya anakabiliwa na mashtaka mawili ambayo ni kujipatia Sh5.1 bilioni na kutakatisha kiasi hicho cha fedha.

Dar es Salaam. Upande wa mashtaka katika kesi ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu inayomkabili Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya JATU PLC, Peter Gasaya (33), wamesema wanasubiri kupangiwa tarehe ya vikao kwa ajili ya kufanya majadiliano ya kuimaliza kesi hiyo.

 Gasaya anakabiliwa na mashtaka mawili likiwemo la kujipatia Sh5.1bilioni na kutakatisha kiasi hicho cha fedha.

Aprili 24, 2023 Gasaya kupitia wakili wake, Nafikile Mwamboma, aliiieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa amemwandika barua ya kukiri na kuomba apunguziwe adhabu, Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP).

Kutokana na hali hiyo, Mahakama hiyo ilitoa muda kwa upande wa mashtaka kuanza majadiliano ya kuimaliza kesi hiyo kwa njia ya majadiliano na DPP.

Hata hivyo, leo Jumatatu Julai 17, 2023 Wakili wa Serikali Eva Kassa, ameieleza Mahakama hiyo, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate kesi hiyo imeitwa kwa ajili ya kutajwa na kwamba wanasubiri kupangiwa tarehe ya kuanza vikao kwa ajili ya kuanza majadiliano ya kuimaliza kesi.

Wakili Kassa amedai kutokana na hali hiyo, wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Kabate baada ya kusikiliza maeneo hayo, ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 31, 2023.

Katika kesi ya msingi, mshtakiwa anakabiliwa na mashtaka mawili ambayo ni kujipatia Sh5.1bilioni na   kutakatisha kiasi hicho katika kesi ya uhujumu uchumi namba 8/2023.