Mlandege yachukuwa mkono kwa Watunisia

Saturday November 28 2020
By Mwandishi Wetu

HALI bado ni tete kwa wawakilishi wa Tanzania upande wa visiwani Zanzibar, baada ya jioni hii

Mlandege kupigwa mabao 5-0 na CS Cfaxien ya Tunisia kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa

Afrika ikiwa ni saa chache tangu KVZ nao kupasuka kwa Wasudan katika Kombe la Shirikisho.

KVZ ilitandikwa bao 1-0 ugenini na Al Atbara na kujiweka katika wakati mgumu kwa mchezo wa

marudiano utakaopigwa wikiendi ijayo mjini Unguja, Zanzibar.

Wakati mashabiki wakiamini KVZ imeteleza tu jana Ijumaa, Mlandege waliwaalika Watunisia na

Advertisement

kufumuliwa mkono na kujiweka katika nafasi finyu ya kupenya kuingia raundi ya kwanza, kwani

mabingwa hao wa visiwani watalazimika kushinda mabao zaidi ya matano ili iwang'oe Cfaxien

kitu ambacho ni ndoto za alinacha, japo kwenye soka lolote linaweza kutokea.

Mabao ya Watunisia yaliwekwa kimiani na Kingsley Eduwo dakika ya 30, Hani Amamou (dk 41)

na hat trick kutoka kwa Firas Chaouat aliyefunga dakika 56, 79 na 84 yaliyoimaliza kabisa

Mlandege ambayo kabla ya pambano hilo ilijitutumua kwamba itawashangaza wageni wao.

Kwenye mechi nyingine za ligi hiyo, Wakenya Gor Mahia walipasuka mabao 2-1 ugenini mbele

ya wenyeji wao APR ya Rwanda, huku Vipers ya Uganda nayo ililala nyumbani 1-0 dhidi ya Al-

Hilal Omdurman ya Sudan.

Musongati inayowakilisha Burundi katika Kombe la Shirikisho nayo ililazimika kupindua meza

kutoka nyuma na kuambulia sare ya 2-2 nyumbani dhidi ya  Green Eagles ya Zambia, huku

Wazambia wenyine wa Forest Rangers ikilazimishwa suluhu nyumbani na Bouenguidi ya Gabon.

Mchezo huo ulikuwa wa Ligi ya Mabingwa ambayo ilishuhudia wapinzani wa Simba ama Plateau

United kwenye raundi ya kwanza, FC Platnum ya Zimbabwe ikishinda ugenini dhidi ya Costa do

Sol ya Msumbiji. Mshindi wa mechi ya Simba na Plateau inayopigwa kesho Jumapili nchini

Nigeria na wa mchezo huo wa Platnum kutoka Zimbabwe na Costa ndo zitakazoumana raundi ya

Advertisement