Mmarekani apandishwa kizimbani Kisutu, akosa dhamana

Muktasari:

  • Raia wa Marekani, Brandon Summerlin amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka la kusafirisha dawa za kulevya Mescaline zenye uzito wa gramu 56.04.

Dar es Salaam. Raia wa Marekani, Brandon Summerlin amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka la kusafirisha dawa za kulevya Mescaline zenye uzito wa gramu 56.04.
Wakili wa Serikali Tumaini Mafuru alisoma shtaka hilo leo Januari 24, 2023 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi alidai kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo Novemba 12, 2022 katika ofisi za Posta wakiwa na dawa hizo.
Baada ya kusomewa shtaka hilo mshitakiwa alikana upande wa mashtaka ulidai upelelezi umekamilika.
Hakimu Shahidi iliahirisha shauri hilo hadi Februari 7, 2023 kwa ajili ya kumsomea mshtakiwa hoja za awali.
Mshitakiwa amekosa dhamana kwa kuwa shtaka hilo halina dhamana kutoka na kiasi cha dawa za kulevya hizo alichokamatwa nacho kimezidi gramu 20.