Mmoja auawa mkoani Kilimanjaro

Wednesday September 15 2021
mmoja auwawapic
By Janeth Joseph

Moshi. Denis Chuwa (21) mkazi wa kitongoji cha Manjaro kata ya Uru Mashariki wilayani Moshi ameuawa na watu wasiojulikana na mwili wake kutelekezwa pembezoni mwa barabara ya kuelekea Uru Shimbwe.

Akizungumza leo Jumatano Septemba 15, 2021 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amesema tukio hilo limetokea jana Jumanne Septemba 14, 2021 na kwamba mwili huo ulikutwa umekatwa na kitu chenye ncha kali.

“Msako mkali unaendelea kuwatafuta waliotenda mauaji ya kijana huyu anayedaiwa kuwa alikuwa na tatizo la akili, inaonekana amekatwa na kitu chenye ncha kali shingoni . mwili wake umehifadhiwa hospitali ya KCMC,” amesema.

Advertisement