Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Moto wateketeza mabanda soko la Tegeta

Muktasari:

Leo Jumanne Februari 18, 2020 moto ambao chanzo chake hakijajulikana umeteketeza vibanda katika soko la Tegeta Nyuki Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam. Leo Jumanne Februari 18, 2020 moto ambao chanzo chake hakijajulikana umeteketeza vibanda saba katika soko la Tegeta Nyuki Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Mwananchi leo Kamanda wa Polisi Kinondoni, Musa Taibu amesema moto huo ulianza saa 6 usiku.

“Ni kweli moto umeshika sehemu ya maduka na sio soko lote, vibanda saba vimeteketea. Baada ya kupata taarifa polisi kwa kushurikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji walifanikiwa kuuzima,” amesema.

Kamanda Taibu amesema uchunguzi umeanza kubaini chanzo na hasara iliyosababishwa na moto huo.

“Bado chanzo hakijafahamika, tunafanya uchunguzi kubaini. Hakuna mtu yeyote aliyepoteza maisha,” amesema.