Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chaumma wamng'oa Mwalimu, Kigaila apewa mikoba

Muktasari:

  • Leo Jumanne, kikao cha Halmashauri Kuu ya Chaumma kimepiga kura ya ndio ya kutokuwa na imani na Katibu Mkuu wake, Salum Mwalimu.

Dar es Salaam. Halmashuri Kuu ya Chama cha Ukombozi wa Umma( Chaumma), imemng'oa aliyekuwa katibu mkuu wa chama hicho, Salum Mwalimu huku ikimkaimisha Benson Kigaila kuongoza wadhifa huo.

Wajumbe 31 wa halmashauri kuu ya Chaumma kwa kauli moja imepiga kura ya ndio ya kutokuwa na imani na Mwalimu wakimtuhumu kwa makosa mbalimbali ikiwamo ya matumizi mabaya ya ofisi na ubadhirifu wa fedha za chama.

Mkurugenzi wa Oganizesheni, Mipango na Uchaguzi, Ismail Kangeta ameliambia Mwananchi leo Juni 30,2026 kuwa kikao kilichomalizika usiku huu  ndio kimefikia uamuzi huo.

"Tumetengua uteuzi wa Mwalimu, tumemkaimisha Kigaila katika nafasi hiyo," amesema Kangeta.

Kabla ya kung'olewa, mapema leo, Mwalimu aliwasilisha barua kwa Mwenyekiti, akiomba kuundwe timu ya kuchunguza tuhuma zinazomkabili na alisema angekuwa tayari kuwa nje ya ofisi kupisha uchunguzi huo.

Miongoni mwa sababu zinazotajwa na wajumbe kutokuwa na imani na kiongozi huyo ni matumizi mabaya ya ofisi, kupongeza ushindi wa CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29 na ubadhirifu wa fedha.


Endelea kufuatilia Mwananchi…