Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mradi Liganga, Mchuchuma kuanza miezi mitatu ijayo

Msemaji wa Serikali na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa

Muktasari:

  • Serikali imeamua kutatua changamoto na malalamiko ya muda mrefu ya wananchi wa Mkoa wa Njombe kutokana na kuchelewa kuanza mradi huo.

Njombe.  Serikali imesema mradi wa makaa ya mawe na chuma wa Liganga na Mchuchuma unaotekelezwa wilayani Ludewa Mkoa wa  Njombe, unatarajia kuanza miezi mitatu ijayo.

Hayo yamesemwa leo  Jumapili Mei 10, 2026 na Msemaji wa Serikali na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa.

Msigwa amesema Serikali imeamua kutatua changamoto na malalamiko ya muda mrefu ya wananchi wa Mkoa wa Njombe kutokana na kuchelewa kuanza kwa mradi huo.

Amesema Serikali ipo zaidi ya asilimia 90 kukamilisha mazungumzo na baada ya miezi mitatu ijayo, wananchi wataanza kuona matokeo ya uwekezaji mkubwa katika mradi wa Liganga na Mchuchuma.

"Huu ni mradi wa kimkakati na kielelezo, ni mradi ambao tunategemea utazalisha ajira zaidi ya 6,500 na ajira zisizo za moja kwa moja zaidi ya 26,000 na itaiwezesha nchi yetu kupata bidhaa ya chuma ya kutosha," amesema Msigwa.

Amesema ndani ya mradi huo utakuwepo uzalishaji wa mradi wa umeme wa Megawatt 600 na kwa sasa mwekezaji anakamilisha taratibu za mwisho ili mradi huo uanze.

Amesema utakuwa na uwezo wa kuzalisha chuma ghafi 2.9 trilioni kwa mwaka na ni mradi ambao utawezesha kuzalisha bidhaa za chuma  tani 1.1 milioni kwa mwaka na mgodi wa makaa ya mawe utazalisha tanimilioni  3 za makaa ya mawe.

Amesema watafiti wamebaini kuwa makaa ya mawe yaliyopo nchini ni zaidi ya tani  bilioni 5na Tanzania ni moja ya nchi yenye makaa mengi ya mawe na bora na yataanza kuzalishwa katika mradi huo wa Liganga na Mchuchuma.

Amesema miaka ishirini na tano ya kwanza ya mradi huo wanategemea Serikali itapata mapato ya Dola 1.9 bilioni za Marekani ni sawa na zaidi ya Sh 5.17 bilioni  kutokana na uwekezaji wa mradi huo.

Mkazi wa Njombe, Nico Luoga amesema kuanza kwa mradi huo kutawanufaisha wananchi wa mkoa huo kwa kupata ajira na kufanya biashara kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu.

"Mradi ukianza ni ukombozi kwetu tutapata ajira na kufanya biashara za mazao na mifugo yetu" amesema Luoga.