Mrema amkumbusha Lowassa mwaka 1992

Lowassa

Muktasari:

“Hata angekuja Lowassa sasa, nitamuuliza mwaka 1992 wakati natoka CCM nilikwambia tutoke sasa maji yamechemka tukiweka unga tutapata ugali, ukagoma Lowassa,” amesema Mrema jana alipozungumza na wanachama wa Chama cha Waendesha Bodaboda Wilaya ya Kinondoni (Chabbowiki).

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Bodi ya Msamaha kwa Wafungwa (Parole), Augustine Mrema amesema Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa angefuata ushauri aliompa wa kuhama CCM mwaka 1992 wangeingia Ikulu, 1995.

“Hata angekuja Lowassa sasa, nitamuuliza mwaka 1992 wakati natoka CCM nilikwambia tutoke sasa maji yamechemka tukiweka unga tutapata ugali, ukagoma Lowassa,” amesema Mrema jana alipozungumza na wanachama wa Chama cha Waendesha Bodaboda Wilaya ya Kinondoni (Chabbowiki).

Mrema amesema Lowassa aliamua kuendelea ‘kula kidogo’ na kuendelea kubaki CCM hadi alipotaka kugombea urais na jina lake kukatwa, akahamia upinzani.