Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mstaafu wa Polisi ajinyonga bafuni

Muktasari:

  • Mstaafu wa Jeshi la polisi nchini,Omary  Charema Msangi mkazi wa Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro  amejiua kwa kujinyonga bafuni kwake  kwa kutumia waya wa pasi kwa madai ya kuuzwa mali zake na mkewe wakati yupo kwenye matibabu.

Moshi. Mstaafu wa Jeshi la Polisi nchini, Omary Charema Msangi amejiua kwa kujinyonga bafuni kwake kwa kutumia waya wa pasi.

Tukio la kujinyonga mstaafu huyo limetokea usiku wa kuamkia jana akiwa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi eneo la Kiboriloni Manispaa ya Moshi ambapo mwili wa mstaafu huyo ulichukuliwa na kupelekwa kuhifadhiwa Hospitali ya Rufaa ya KCMC.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa  amethibitisha kutokea kwa  tukio leo Jumatano Januari 26, 2022 akisema bado wanaendelea na uchunguzi wa kubaini chanzo cha kujinyonga kwa mstaafu huyo.

"Ni kweli hili tukio limetokea na tunafuatilia kujua hasa chanzo cha kujinyonga kwake," amesema Kamanda Maigwa

Taarifa za chanzo cha  kijinyonga kwa  askari huyo kutoka kwa mmoja wa ndugu wa familia hiyo zinadai kuwa wakati mwanaume huyo akiwa kwenye matibabu mkoani Dar es salaam, mke wake alitumia nafasi hiyo kuuza mali zake zote ikiwa ni nyumba, mashamba pamoja na mali nyingine.

Inadaiwa kuwa baada ya mtaafu huyo kurejea nyumbani kutoka kwenye matibabu alikuta nyumba yake imeuzwa na kulazimika kwenda kupanga.

Mwili wa mwanaume huyo unatarajiwa kuzikwa leo  Usangi Wilaya ya Mwanga.