Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtendaji wa Kijiji na wenzake wanne kizimbani wa kuuza shamba

Mtendaji wa Kijiji cha Mboliboli na wenzake wanne wakiwa wapi mahakama ya Mkoa wa Iringa kwa tuhuma za kuuza shamba kinyume na sheria za kijiji cha Mboliboli Pawaga mkoani Iringa. Picha na Takukuru Iringa

Muktasari:

  • Watuhumiwa hao watano kutoka Kijiji cha Mboliboli, Wilaya ya Iringa, pamoja na wakazi wanne wa kijiji hicho wamefikishwa mahakama ya mkoa wakituhumiwa kutumia nyadhifa na mazingira yao kuuza shamba linalodaiwa kumilikiwa na mwananchi mwingine na kujipatia Sh12.6 milioni.

Iringa. Aliyekuwa Kaimu Mtendaji wa Kijiji cha Mboliboli, Wilaya ya Iringa, Amini Mwakisambwe, pamoja na wakazi wanne wa kijiji hicho wamefikishwa katika Mahakama ya Mkoa wa Iringa wakikabiliwa na makosa mbalimbali ya rushwa, matumizi mabaya ya madaraka na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu baada ya kudaiwa kuuza shamba ambalo hawakuwa na mamlaka ya kisheria kulimiliki.

Washtakiwa hao walifikishwa mahakamani Juni 22, 2026 katika Kesi ya Uhujumu Uchumi Na. 13895/2026 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Mkoa wa Iringa, Honorious Kando.

Mbali na Mwakisambwe, washtakiwa wengine ni Festo Kizumbe, Agustino Mkomola, Abdallah Nguswa na Katalai Mgoboleni, wote wakazi wa Kijiji cha Mboliboli.

Mtendaji wa Kijiji cha Mboliboli na wenzake wanne wakiwa wapi mahakama ya Mkoa wa Iringa kwa tuhuma za kuuza shamba kinyume na sheria za kijiji cha Mboliboli Pawaga mkoani Iringa. Picha na Takukuru Iringa

Upande wa mashtaka, ukiongozwa na mawakili wa TAKUKURU Mkoa wa Iringa, Salum Bhoki na Lisa Kasongwa, ulieleza mahakama kuwa kati ya Februari na Machi mwaka 2022, Mwakisambwe akiwa Kaimu Mtendaji wa kijiji hicho alishirikiana na washtakiwa wenzake kuuza shamba lenye ukubwa wa ekari 28 kwa mfanyabiashara Furahini Vahaye.

Kwa mujibu wa maelezo ya mashtaka, shamba hilo linadaiwa kuwa mali halali ya Sinzo Masanja na lina hati ya hakimiliki ya kimila, huku washtakiwa wakidaiwa kutokuwa na umiliki wa kisheria wa eneo hilo.

Mahakama ilielezwa kuwa kupitia mauziano hayo, washtakiwa walijipatia jumla ya Sh12.6 milioni kwa kuuza ardhi ambayo haikuwa mali yao.

Mtendaji wa Kijiji cha Mboliboli na wenzake wanne wakiwa wapi mahakama ya Mkoa wa Iringa kwa tuhuma za kuuza shamba kinyume na sheria za kijiji cha Mboliboli Pawaga mkoani Iringa. Picha na Takukuru Iringa

Mwakisambwe anakabiliwa na shtaka la matumizi mabaya ya madaraka pamoja na kusaidia kutenda kosa, huku washtakiwa wenzake wakishtakiwa kwa kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Baada ya kusomewa hati ya mashtaka, washtakiwa wote walikana makosa yanayowakabili na mahakama iliwapa dhamana baada ya kuridhika kuwa wametimiza masharti yaliyowekwa, huku kesi hiyo ikiahirishwa hadi Julai 17, 2026 kwa ajili ya kusomwa hoja za awali.