Munkunda awapongeza Benki ya Akiba kwa kutoa elimu ya fedha

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mwanahamisi Munkunda akizungumza wakati alipotembelea banda la Akiba Bank aliyevaa fulana nyeusi ni Afisa Masoko ya Akiba Benki Anthony Kunambi akimweleza Mkuu wa Wilaya huyo fursa zinazopatikana katika benki hiyo.

Muktasari:

  • Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mwanahamisi Munkunda aipongeza benki ya Akiba kwa kuwa mstari wa mbele kutoa elimu ya fedha kwa vijana, akihimiza benki nyingine kuwaiga benki ya hiyo ili kuhakikisha zinakuwepo fursa mbalimbali za kiuchumi.

Dar es Salaam. Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mwanahamisi Munkunda ameipongeza benki ya Akiba kwa kuwa mstari wa mbele kutoa elimu ya fedha kwa vijana, hususan katika nyanja ya kujiwekea akiba, huduma za mikopo, mpango wa fedha na kupanga bajeti za matumizi binafsi na Biashara ili kusaidia kukuza Uchumi wao.

Munkunda ameyasema hayo, Mei 24, katika tamasha la vijana linalojulikana kama "Kijana Janjaruka" lililoandaliwa na Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, viwanja vya Zakhem-Mbagala ambapo benki ya Akiba ilishiriki kikamilifu.

Wakati alipotembelea banda la benki ya akiba, ameeleza jinsi alivyo furahishwa na huduma zao "Naishukuru benki ya Akiba kwa kuonyesha mfano wa kuigwa kwa kutoa huduma bora katika jamii, hivyo nina ahidi kuendelea kushirikiana na taasisi za fedha hususan mabenki katika kuchochea maendeleo endelevu ndani ya Manispaa ya Temeke na Taifa kwa ujumla” amesema

Pamoja na hayo, mkuu huyo wa wilaya amefanikiwa kujionea fursa iliyozinduliwa na benki ya Akiba akaunti maalum kwa ajili ya Wanawake inayoitwa akaunti ya ‘WARIDI’ ambayo ina masharti nafuu sana ya uendeshaji, huku lengo likiwa ni kuwainua wanawake katika kufikia ndoto zao za mafanikio katika ujasiriamali.

Tamasha hilo lilikua na lengo la kutoa fursa mbalimbali za kiuchumi kwa vijana na maeneo ya jirani, kualika taasisi za fedha hususan mabenki ili kutoa elimu ya fedha kwa vijana.