Musk asimamisha mpango wa kuinunua Twitter

Friday May 13 2022
twitterpiic
By Mwandishi Wetu

New York, Marekani (AFP). Elon Musk amesema leo Ijumaa kuwa amesimamisha kwa muda mpango wake unaosubiriwa kwa hamu wa kuinunua Twitter, na kusababisha thamani ya hisa za mtandao huo mkubwa wa kijamii kuporomoka.


"Mpango wa Twitter kwa muda umesimama kutegemea taarifa za mahesabu kwamba akaunti hewa au za kughushi zinawakilisha chini ya asilimia 5 ya watumiaji," ameandika katika akaunti yake ya Twitter.


Musk, mtu tajiri kuliko wote duniani na muasisi wa kampuni ya kutengeneza magari ya Tesla, aliamua kuhakikisha anaondoa akaunti feki, ikiwa ni sehemu kubwa katika mpango wake wa kuinunua Twitter kw adau la dola 44 bilioni.

Wakati mpango huo ulipotangazwa mwishoni mwa Aprili alisema alitaka kuifanya Twitter kuwa "bora kuliko wakati mwingine wowote" kwa kuondoa na kuhakikisha watumiaji ni binadamu halisi.

Advertisement