Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Muuguzi, dereva gari la wagonjwa wafa ajalini

Muuguzi, dereva gari la wagonjwa wafa ajalini

Muktasari:

  • Muuguzi wa zahanati ya Kisiwani na dereva wa gari la wagonjwa wamefariki dunia baada ya gari hilo kupinduka wakati wakimuwahisha mgonjwa hospitali.

Same. Muuguzi wa zahanati ya Kisiwani na dereva wa gari la wagonjwa, wamefariki dunia baada ya gari hilo kupinduka na kupoteza mwelekeo wakati wakimuwahisha mgonjwa Hospitali ya Wilaya ya Same.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha leo Agosti 8, 2021 kutokea kwa ajali hiyo jana jioni  katika barabara ta Same kisiwani, eneo la Majevu, Kata ya Kisima,  wilayani Same.

Amewataja waliofariki dunia kuwa ni muuguzi wa zahanati hiyo, Joshua Methew (29) na dereva  Jumanne Makumbe (48).

Wengine ambao wamejeruhiwa ni Ester Laizer (35), Magdalena Kuvaa (45) na Paresetwi Peutu (50).

Kamanda Maigwa amesema chanzo cha ajali hiyo ni gari hilo kupasuka tairi la nyuma na kupoteza mwelekeo kisha kupinduka.

"Gari hili lilikuwa likitokea zahanati ya Kisiwani kuelekea Hospitali ya Wilaya ya Same likiwa limebeba mgonjwa. Lilipasuka tairi la nyuma na kupoteza mwelekeo na kutoka nje ya barabara na kupinduka," amesema Kamanda Maigwa.

Amesema miili ya marehemu imehifadhiwa Hospitali ya Wilaya ya Same na majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo.

Imeandikwa na Janeth Joseph na Dickson Mzanva