Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mvua yabomoa nyumba 140 Kigoma

Kigoma. Zaidi ya wananchi 250 wa Kata ya Herembe Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma hawana mahala pa kuishi baada zao nyumba 140 kuezuliwa na upepo, kubomoka kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani humo.

Mbali na nyumba, pia zahanati ya Herembe na ofisi ya mtendaji wa kijiji zimeezuliwa na kubomoka huku mashamba ya wananchi yaliyokuwa na mazao yakijaa maji na kuharibika.

Akizungumza leo Jumapili Desemba 31, 2023 Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Uvinza ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Salim Kali amesema tukio hilo limetokea Desemba 29, 2023 na kuwataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari wakati kamati ya maafa ikifanya tathmini ya tukio hilo na namna yakuwasaidia waathirika.

“Wananchi ambao nyumba zao zimebomoka wasiingie kwenye nyumba hizo na badala yake waombe hifadhi ya muda kwa baadhi ya watu ambao nyumba zao zimebakia wakati Serikali ikiendelea na tathmini kuhusiana na maafa hayo,”amesema Kali.

Muuguzi katika zahanati ya Herembe, Devotha Pascal amesema baadhi ya dawa na vifaatiba vilivyokuwepo katika zahanati hiyo vimeharibika na vingine vimesombwa na maji.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kalelankwasi, Issa Hamisi amesema mvua hizo pia zimeharibu daraja lililokuwa linatumika na wanafunzi kama kivuko kwenda shuleni.

“Niombe Serikali ifanye haraka kujenga daraja, kwani muda si mrefu wanafunzi wanafungua shule na kama daraja halitakuwa limekamilika basi wanafunzi watashindwa kwenda kusoma,”amesema Hamisi,

Pia ameiomba Serikali iwasaidie wananchi waliopatwa na maafa hayo, kwani mali na vitu vyao walivyokuwa navyo vimeharibika na hawana njia nyingine kwa wakati huu ambayo itawasaidia, hivyo macho yao yote yapo kwa Serikali.