Mwanafunzi amchoma visu hadi kufa mwanafunzi mwenzake

Kamanda wa polisi Tarime/Rorya Kamishina msaidizi Mwandamizi, Henry Mwaibamba
Muktasari:
Marehemu alikuwa ni mkazi wa Iganana, kata ya Sabasaba, Tarime.
Tarime. Mwanafunzi wa darasa la tano, shule ya msingi, Azimio, Tarime, Charles Mathias (15) amekamatwa na polisi kwa tuhuma za kumchoma kisu na kumuua, mwanafunzi mwenzake Rhobi Chacha(14)
Kamanda wa polisi Tarime/Rorya Kamishina msaidizi Mwandamizi, Henry Mwaibamba amesema tukio hilo limetokea Juni 25 saa nne asubuhi na Rhobi alifariki dunia saa sita mchana wakati akipata matibabu Hospitali ya mji wa Tarime.
Marehemu alikuwa ni mkazi wa Iganana, kata ya Sabasaba, Tarime.
“Mtuhumiwa baada ya kutendo kitendo hicho alikimbia na jeshi la polisi linafanya juhudi kumtafuta ili sheria ichukue mkondo wake,”amesema Kamanda.
Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mji wa Tarime, Innocent Kweka, amesema alimpokea Rhobi, saa nne asubuhi alimpokea lakini alifariki dunia wakati akiendelea na matibabu.
“Kwenye uchunguzi ilibainika kuwa alichomwa na kitu chenye incha kali na kilizama kwenye mapafu hali iliyosababisha marehemu kuvuja damu na kupoteza maisha,”amesema Kweka.
Akizungumzia tukio hilo Mwalimu Mkuu Msaidizi Shule ya Msingi Azimio amesema Rhobi na Charles wanasoma shule moja.
“Inasikitsha sana, mtuhumiwa alikuwa anatarajia kufanya mtihani wake wa mwisho wa darasa la saba,” amesema
Mwenyekiti wa Mtaa wa Iganana kata ya Sabasaba, Edward Thomas alisema mtuhumiwa na marehemu ni majirani wanaotenganishwa na barabra ya mtaani.
“Ulizuka ugomvi kati yao wakati wanacheza mpira ambapo mtuhumiwa aliingia nyumbani na kuchukua kisu na kuanza kumshambulia marehemu na hivyo kupelekea kifo chake,”amesema Thomas