Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwanafunzi UDSM akamatwa kwa madai ya kutoa taarifa za uongo za corona

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Debora Magiligimba

Shinyanga. Jeshi la polisi mkoani Shinyanga linamshikilia mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dare es Salaam mwaka wa tatu katika  kitivo cha Kiswahili kwa kosa la kusambaza kwenye mitandao ya kijamii taarifa za uongo kuhusu ugonjwa wa corona.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Debora Magiligimba amemtaja mwanafunzi huyo kuwa ni Mariamu Jumanne Sanane (23) ambaye alikamatwa Aprili 9, mwaka huu usiku katika  eneo la mtaa wa Tabora katika Mgodi wa Almasi wa Mwadui wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.

Kamanda Magiligimba amesema mnamo  Machi 26 mwaka huu askari wa
kikosi kazi cha mitandao ya kijamii walifanikiwa kuona ujumbe kwenye
mtandao wa whatsap uliotumwa na mtuhumiwa ukisomeka, “…Mpk ss
Tanzania ina wagonjwa wapatao takriban 230 wa COVID 19 na waliofariki
ni 04.”

Mtuhumiwa baada ya kupekuliwa alikutwa na simu iliyotumika kutuma
ujumbe huo ambapo tayari amehojiwa na anatarajiwa kufikishwa
mahakamani kwa makosa ya kuchapisha na kusambaza taarifa za uongo mitandaoni na kutoa takwimu za uongo.

“Nitoe wito kwa wananchi wote kuwa makini na matumizi ya
mitandao ya kijamii na waache kupotosha watu kwani kufanya hivyo ni
kosa la jinai watachukuliwa hatua Kali za kisheria,” alisisitiza Magiligimba