Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwanza wazindua kampeni ya ‘Afya yangu, Furaha Yangu’

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu

Mwanza.Mkoa wa Mwanza umezindua kampeni ya ‘Afya Yangu Furaha Yangu’ inayolenga kuhamasisha upimaji virusi vya Ukimwi.

Akizungumza leo Julai 21 wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Mratibu wa Ukimwi Mkoa wa Mwanza Dk Pius Masele amesema maambukizi ya virusi vya ukimwi yameongezeka na kufikia asilimia 7.2 kutoka asilimia 4.2, mwaka 2011

 Kwa mujibu Dk Masele amesema ongezeko hilo linaufanya mkoa huo kuwa wanne ukitanguliwa na Njombe,Iringa na Mbeya.

Dk Masele ameeleza mikakati ya kupunguza maambukizi hayo ni  kuzifikia 90 tatu, ifikapo kwama 2030.

Amesema 90, 90, 90 zinamaanisha kupunguza maambukizi ya Ukimwi kwa asilimia 90 ifikapo 2030, asilimia 90 ya wananchi kupima ifikapo mwaka huo na asilimia 90 kuanza kutumia dawa za kufubaza makali ya Ukimwi.