Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwenye ulemavu ataka elimu ya mikopo ya halmashauri

Mkazi wa Whangani West, Yusuph Rajabu aliyepata mkopo wa Sh2 milioni ambayo ni kutoka asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Manispaa kwa ajili ya mikopo ya wanawake, vijana na walemavu. Picha na Florence Sanawa

Muktasari:

  • Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Dunstan Kyobya ndiye aliyekabidhi mfano wa hundi ya zaidi ya Sh244.86 milioni kwa vikundi 35 vya wajasiriamali katika Manispaa ya Mtwara Mikindani jana Desemba 15 mkoani hapa.

S:



Florence Sanawa, Mwananchi


Mtwara. Yusuph Rajabu mwenye ulemavu anayeishi Manispaa ya Mtwara, ameshukuru kuwa miongoni mwa watu waliopata mikopo ya halmashauri inayotolewa kwa wanawake, vijana na wenye ulemavu, akitaka elimu zaidi itolewe katika matumizi ya mikopo hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Dunstan Kyobya ndiye aliyekabidhi mfano wa hundi ya zaidi ya Sh244.86 milioni kwa vikundi 35 vya wajasiriamali katika Manispaa ya Mtwara Mikindani jana Desemba 15 mkoani hapa.

Akizungumza na Mwananchi baada ya hatua ya kukabidhi mikopo hiyo, Yusuph Rajabu, Mkazi wa Shangani West aliyepata mkopo wa Sh2 milioni, amesema kuwa watu wenye ulemavu wanapaswa kuelimishwa juu ya mikopo hiyo ili waweze kujikomboa kimaisha.

Amesema amekuwa akifuga kuku kwa muda mrefu, lakini hakufahamu kuhusu mikopo hiyo, lakini sasa ameona mafanikio yake.

“Nimepokea mkopo wa Sh2 milioni baada ya kuomba, mimi nilitembelewa na watendaji wa mtaa wakanielimisha juu ya mikopo hiyo nikaamua kuomba

“Unajua makundi mengi ya watu wenye ulemavu yako nyuma kwa kuwa watu wengi hawaamini kama wanaweza kupata mikopo hivyo mwitikio kuwa mdogo kwa sas anna kuku 200 bado sijaanza kuuza,” amesema.  

Akizungumza katika makabidhoano ya mikopo hiyo, Meya wa Manispaa ya Mtwara Mikindani, Shadida Ndile amesema kuwa wamekabidhi hundi kwa ajiliya vikundi 35 vilivyopewa mkopo na Manispaa ya Mtwara Mikindani.

“Leo tunakabidhi hundi kwa wajasirimali kama seriklai ilivyooagiza kwenye mapato ya ndani kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wanawke vijana na makundi maluma sisi tunatekeleza kwa vitendo,” amesema.

Naye Kaimu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Jemson Mwampiki, amesema kuwa Oktoba 2022 halmashauri ilipokea maombi ya mkopo ya vikundi 52 yenye thamani ya zaidi ya Sh503.97 milioni na baada ya kufanya uhakiki vikundi 48 vilikidhi vigezo vya kupata mkopo wenye ya Sh361.7 milioni.

Hata hivyo, kutokana na upungufu wa fedha vikundi 13 vilivyokosa mikopo ya Sh116.84 milioni vitapatiwa mkopo kwa awamu nyingine kwa kadiri fedha zitakavyokuwa zinapatikana.