Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwili wa aliyeuawa Israel kuwasili kesho

Kijana Clemence Mtenga enzi za uhai wake.

Muktasari:

  • Mwili huo ambao uliagwa nchini Israel Novemba 22, 2023 na kushuhudiwa na baadhi ya Watanzania, unatarajiwa kuzikwa Jumanne ya Novemba 28 nyumbani kwao katika Kijiji cha Kirwa Mashati, Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro.

Moshi. Mwili wa Clemence Mtenga (22), Mtanzania aliyeuawa nchini Israel, unatarajiwa kuwasili nchini Kesho Jumamosi Novemba 25, 2023 saa 2 usiku, kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia).

Mwili huo ambao uliagwa nchini Israel Novemba 22, 2023 na kushuhudiwa na baadhi ya Watanzania, unatarajiwa kuzikwa Jumanne ya Novemba 28, 2023 nyumbani kwao katika Kijiji cha Kirwa Mashati, Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro.

Msemaji wa Familia hiyo, Boniphace Mtenga amesema baada ya kuupokea mwili pale Kia, wataenda kuuhifadhi katika Hospitali ya Huruma iliyopo wilayani Rombo huku wakisubiri taratibu za maziko.

"Taarifa tuliyoipata kutoka wizarani, tayari mwili umeondoka Israel, na tumeambiwa mwili utaingia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kia, saa 2 usiku Jumamosi ya Novemba 25, ambapo familia tutakuwepo kupokea," amesema Mtenga.

Mtenga ambaye pia ni Mwenyekiti wa ukoo wa Mtenga amesema: "Baada ya kuupokea Kia, tutausafirisha hadi Hospitali ya Huruma iliyoko wilayani Rombo ambapo utahifadhiwa hapo hadi Jumanne ambapo ndiyo siku tutafanya maziko kumuhifadhi ndugu yetu."

Akielezea ratiba ya siku ya maziko, amesema Jumanne baada ya kuutoa mwili hospitalini, utapelekwa nyumbani ambapo utaagwa na familia, kisha saa 4:30 asubuhi utapelekwa kanisani, parokia ya Mashati ambapo ibada ya maziko itafanyika na baada ya ibada utarudishwa nyumbani kwaajili maziko.

Novemba 17, 2023  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ilithibitisha kupokea taarifa za kifo cha Clemence Mtenga, ambaye ni mmoja kati ya Watanzania wawili ambao pamoja na raia wa mataifa mengine walikuwa hawajulikani walipo baada ya kuanza kwa vita kati ya Hamasi na Israel.

Taarifa hiyo iliyotolewa na kitengo cha mawasiliano ya serikali cha Wizara hiyo, ilieleza Clemence alikuwa miongoni mwa vijana wa kitanzania 260, waliokwenda Israel kushiriki mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa vitendo, chini ya mpango wa ushirikiano kati ya serikali ya Tanzania na Israel.

Marafiki, ndugu wazungumza

Baltazary Mtenga ambaye ni kaka wa marehemu, amesema kikubwa wanachosubiri kwa sasa ni kuona mwili wa ndugu yao, ili kujiridhisha na kuuhifadhi katika nyumba yake ya milele.

"Clemence ni mdogo wangu, maana ni mtoto wa babangu mdogo, kiukweli tumepata pigo kubwa sana kama familia lakini tunaamini ni kazi ya Mungu, kikubwa tunachoomba na kusubiri kwa sasa ni kuuona mwili wake angalau turidhike kidogo na tumzike nyumbani," amesema Mtenga.

Ameongeza kuwa: "Alikuwa kijana muungwana sana na tuliyeheshimiana na aliniamini sana kama kaka yake, hatuna cha kusema maana tayari ametutoka na kutuacha." 

Naye Jackson Mroso ambaye ni rafiki wa marehemu, amesema kifo hicho kimewaumiza kama vijana maana ameondoka mapema kabla hawajafurahia ujuzi wake alioupata chuoni.

"Tumepokea msiba huu kwa masikitiko makubwa, alikuwa ni rafiki na ndugu yetu wa karibu ambaye tuliwasiliana hata alipokuwa Israel, lakini kuanzia Oktoba 7, alikuwa hapatikani hadi tukafika kwa baba yake kuuliza, lakini kwa sasa hatuna namna, tuombe tu mwili wake ufike ili tuuage na tuuzike," amesema Mroso.