Mwili wa padre waokotwa Mbeya

What you need to know:

  • Mwili wa padre wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mbeya wa Shiriki wa Wasionari wa Afrika (White Father), Michael Samson umeokotwa jijini Mbeya.

Mbeya. Mwili wa padre wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mbeya wa Shiriki wa Wasionari wa Afrika (White Father), Michael Samson umeokotwa jijini Mbeya.

Mwili huo umeokota katika mto Meta meaneo ya Sabasaba jijini humo Jumamosi Juni 11, 2022.

Taarifa iliyotolewa na Askofu Mkuu wa jimbo hilo na Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Gervas Nyaisonga imeleza Padre Samson alitoweka Ijumaa Juni 10 mwaka huu katika kituo cha Vijana cha Kanisa Katoliki Mbeya saa 12.30 jioni.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa mara baada ya kutoweka juzi mwili wake umeokotwa jana.

“Alitoweka Juni 10, 2022 katika kituo cha Vijana cha Kanisa Katoliki Mbeya majira ya saa 12.30 jioni na mwili wake kupatikana Juni 11, 2022 saa 4:00 asubuhi maeneo ya Sabasaba jijini Mbeya” imesema taarifa hiyo ya Askofu.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio wamedai kuwa mwili huo ulikuwa umefungwa kwenye blanketi.