Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Naibu Waziri ahimiza wazazi kusimamia elimu ya watoto wao ipasavyo

Sumbawanga. Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Deus  Sangu ameonesha kuumizwa na mwitikio mdogo wa elimu mkoani Rukwa  huku akiwaonya wazazi wenye tabia ya kuwaelekeza watoto wao  kujikosesha au kuchora picha katika  mitihani yao kwa lengo la kujihusisha na shughuli za kilimo na ufugaji.

Sangu ambaye pia ni Mbunge wa Kwela  ametoa kauli hiyo leo Februari 24, 2025 wakati alipotembelea na  kuzungumza na  wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Miangalua  iliyopo katika wilaya ya  Sumbawanga, mkoani Rukwa.

Amesema Serikali amefanya  uwekezaji mkubwa wa  miundombinu ya elimu huku akitaja ujenzi shule za  sekondari kila kata pamoja na Shule  ya Wasichana ya  Rukwa,  lengo ni kuhakikisha hakuna mtoto anayeachwa nyuma.

Hata hivyo, Sangu amesema kutokana na msukumo mdogo kutoka kwa wazazi, watoto walio wengi wamekuwa wakiishia darasa la saba na wale wanaoendelea na sekondari wamekuwa hawafanyi vizuri kwenye mitihani yao ya mwisho.

Kufuatia hali hiyo, Sangu amesema mkoa huo umekuwa kinara kwa idadi kubwa ya watoto wa kike kukatishwa masomo kutokana na kupata mimba, utapiamlo pamoja  na tabia ya  utapeli.

Amesisitiza kuwa elimu ndio injini ya maendeleo ya familia yoyote na kutoa angalizo kwa wazazi kuwa yoyote anayecheza na elimu ya mtoto wake atabaki kuwa nyuma huku fursa za kiuchumi za mkoa huo zikiendelea kuporwa na wananchi wa mikoa mingine.

"Mkoa wa Rukwa umejaaliwa rasilimali za kila aina ikiwemo madini pamoja kuwa ya pili kwa kuzalisha chakula lakini hali zetu ni duni kutokana na kukosekana kwa elimu" amesisitiza Sangu

Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Miangalua, Didas Kayanda amesema jamii yoyote iliyostarabika ni lazima ikumbatie elimu, hivyo amewataka waumini hao kuwa mstari wa mbele kuwahimiza watoto wao juu ya umuhimu wa elimu.

Amesema wazazi ambao hawapeleki watoto shule wachukuliwe hatua kali za kisheria ili iwe funzo kwa wazazi wengine huku akisema Serikali imejitahidi sana kujenga shule nyingi katika Jimbo la Kwela tofauti na hapo awali.