Naibu Waziri kuongoza hafla ya kuaga miili ya wanafamilia watatu
Muktasari:
- Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi, kuongoza hafla ya kuaga mili ya wanafamilia watatu waliopoteza maisha Kwa ajali ya gari Agosti 2 Mwaka huu Bagamoyo.
Dar es Salaam. Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila wanaotarajiwa kuongoza waombolezaji, kuaga miili ya wanafamilia watatu kati ya wanne waliofaliki katika ajali ya gari.
Kwa mujibu wa mshehereshaji (MC) wa shughuli hiyo, Aminata Juma, kutoka Shirika la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), kiongozi mwingine ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro.
Shughuli hiyo inahusisha kuaga miili ya wanafamilia ahao ambao ni Sia Msuya, Dk Norah Msuya na Diana Msuya, waliopoteza maisha katika ajali iliyotokea wilayani Chalinze usiku wa Agosti 2, Mwaka huu wakiwa safarini kuelekea msibani wilayani Same.
"Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro ni baadhi ya viongozi wa kiserikali tunaotegemea kuwapokea," amesema Aminata
Neech ambaye ndiye alikua kaka pekee katika familia hiyo, na ndiye aliyekuwa dereva wa gari hiyo, alizikwa Agosti 6 kijijini kwao Msangeni Ugweno Wilaya ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro.
Na leo Agosti 8 ndiyo siku ambayo ndugu waliosalia watazikwa katika makaburi ya Ununio kwa Kondo baada ya kuagwa katika viwanja vya gofu Kawe jijini Dar es Salaam.