Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Najim, mkewe wafikisha siku 149 gerezani

Mshtakiwa Najim Mohamed, anayekabiliwa na mashtaka mawili ya kusafirisha dawa za kulevya zenye uzito wa kilo 3,050 akiwa chini wa ulinzi wa askari Magereza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Picha na Maktaba

Muktasari:

  • Washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa kusafirisha dawa hizo Desemba 15, 2023 eneo la Kibugumo Shule, Wilaya ya Kigamboni

Dar es Salaam. Najim Mohamed (52) na mkewe Maryam Najim Mohamedi (50) pamoja na  mfanyakazi wa ndani wa kiume, Juma Mbwana Abbas (37), wamefikisha siku 149, wakiwa rumande  bila upelelezi wa kesi yao ya kusafirisha kilo 3,050 za dawa za kulevya kukamilika.

Washtakiwa hao wanaendelea kusota rumande kutoka na mashtaka ya kusafirisha dawa za kulevya na za uhujumu uchumi kutokuwa na dhamana kwa mujibu wa sheria.

Mohamed na wenzake anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka mawili ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroini na Methamphetamine katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisitu.

Kwa mara ya kwanza, washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo, Desemba 29, 2023 na kusomewa kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka hayo mawili.

Tangu siku hiyo, hadi leo Mei 27, 2024, kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa, washtakiwa hao wamefikishwa siku 149, sawa na miezi mitano wakiwa mahabusu, kutokana na upelelezi wa shauri hilo kutokukamilika.

Awali, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Grace Mwanga aliieleza Mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Aaron Lyamuya kuwa upelelezi wa shauri hilo bado unaendelea, hivyo wanaomba tarehe nyingine ya kutajwa.

"Mheshimiwa hakimu, kesi hii imeitwa kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wake bado haujakamilika, hivyo tunaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa na kuangalia umefikia wapi"

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Lyamuya alikubaliana na ombi hilo na kuahirisha kesi hiyo hadi Juni 10, 2024 itakapotajwa na kuwa washtakiwa wanaendelea kubaki rumande.

Kesi hiyo imesikilizwa kwa njia ya video huku washtakiwa hao wakiwa rumande.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa  Desemba 15, 2023 katika eneo la Kibugumo Shule lililopo wilaya ya Kigamboni, walisafirisha dawa za kulevya aina ya heroini yenye uzito wa kilo 882.71.

Shtaka la pili, siku na eneo hilo, washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa kusafirisha dawa za kulevya aina ya Methamphetamine zenye uzito wa kilo 2167.29.