Ndayiragije atakiwa kubadili mfumo Stars

Ndayiragije atakiwa kubadili mfumo Stars

Muktasari:

  • Kocha wa Taifa Stars, Etienne Ndayiragije amesema licha
  • ya kufungwa na Zambia katika mchezo wa kwanza wa mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani (Chan), bado kikosi chake kina nafasi ya kusonga mbele.

Dar es Salaam. Kocha wa Taifa Stars, Etienne Ndayiragije amesema licha

ya kufungwa na Zambia katika mchezo wa kwanza wa mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani (Chan), bado kikosi chake kina nafasi ya kusonga mbele.

Mabao mawili ya kipindi cha pili yalitosha kukipa kikosi cha kocha Milutin Sredojević ‘Micho’ ushindi wa 2-0 na kuifanya Taifa Stars kuwa na kazi ya kufanya katika michezo yote miwili iliyobaki ya Kundi D.

Kama inahitaji kutinga hatua ya robo fainali ya mashindano hayo

makubwa ya Afrika, itahitaji kuanza kwa ushindi katika mchezo wa Jumamosi dhidi ya Namibia, kabla ya kuivaa Guinea Januari 27.

Kocha wa Taifa Stars, Ndayiragije alisema: Tumesikitishwa na kupoteza mchezo wa kwanza, lakini bado hatujatoka katika mashindano, tuna

mechi mbili za kucheza.

“Ulikuwa ni mchezo mgumu wa kwanza, ambao kila timu ilihitaji ushindio, lakini tulipoteza umakini kipindi cha kwanza huku pia tukishindwa kutumia nafasi zetu tulizotengeneza.”

Kocha wa Zambia, ambaye aliwahi pia kuifundisha Yanga, Micho, alisema:

“Kushinda mchezo wa kwanza siku zote unakuwa na furaha, lakini haikuwa kazi nyepesi mbele ya Tanzania,” alisema.

Kipigo hicho kimevuta hisia tofauti kwa wadau wa soka nchini, ambao wengi wao waliiona Taifa Stars katika wakati mgumu wa kusaka ushindi katika mechi mbili za mwisho za kuamua hatima yao Chan.

Kocha Abdul Mingane alisema kwa namna alivyoiangalia mechi hiyo, Stars ilicheza vizuri kipindi cha kwanza na kipindi cha pili hawakusoma wapinzani wao.

“Kuna haja ya kocha kubadili kikosi chake na mfumo, kwani mfumo alioutumia na wachezaji alionao ni vitu viwili tofauti.

“Sijawahi kumuona Kaseke akicheza namba 10 tangu akiwa Mbeya City na hata Yanga, lakini jana (juzi) amecheza hivyo Stars, kama akiweza mechi ijayo aweke washambuliaji wawili.

“Pia nilitegemea kumuona Nyoni angekuepo kikosini kutokana na uzoefu wake, Ndemla pia nilimtegemea angeingia kama ‘sub’ kuchukua nafasi ya

Majogoro kwa kuwa ana uwezo wa kumiliki mpira, lakini ilikuwa tofauti, hata Tshabalala hakustahili kuachwa,” alisema kocha Mingange.

Nyota wa zamani wa Simba, Mtemi Ramadhan alisema Taifa Stars kwanza haipaswi kufikiria matokeo ya mechi iliyopita kama inahitaji kusonga mbele.

“Mechi ijayo wacheze kama ndiyo wanaanza, lakini kuna haja ya mabeki wetu kuongeza umakini zaidi, kama bao la pili tulilofungwa, Kapombe hakuwa makini tu, na mara nyingi tunafungwa mabao ya aina hiyo, hata Yondani iliwahi kumtokea.

Alisema mabeki wanapaswa kuwa makini zaidi si tu kuangalia eneo unapokwenda mpira, bali pia kujua ni nani ambaye yuko nyuma yao wakiwa na mpira.