Ndoa ya Dk Mwaka na Queen yavunjika

Muktasari:

Ndoa ya mtaalamu wa tiba mbadala, Juma Mwaka maarufu Dk Mwaka na mkewe Queen Masanja imevunjwa rasmi leo Jumatano, Januari 25, 2023.

  

Dar es Salaam. Ndoa ya mtaalamu wa tiba mbadala, Juma Mwaka maarufu Dk Mwaka na mkewe Queen Masanja imevunjwa rasmi leo Jumatano, Januari 25, 2023.

Ndoa hiyo imevunjwa baada ya kikao cha Kamati ya Masheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam chini ya uenyekiti wa sheikh wa mkoa, Alhadi Mussa Salum kuketi kwa dharura na kuridhia maombi ya Queen kutaka apewe talaka.

Kwa habari zaidi endelea kufuatilia mitandao yetu ya kijamii na kusoma gazeti la Mwananchi kesho Alhamisi Januari 26, 2023.