Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Necta yatangaza matokeo kidato cha sita 2026, ufaulu waongezeka

Dar es Salaam. Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) limesema jumla ya watahiniwa 124,603 sawa na asilimia 99.56 wamepata ufaulu mzuri wa daraja kwanza hadi la tatu.

Kati ya watahiniwa hao wengi wamepata madaraja ya juu zaidi ambapo watahiniwa waliopata daraja la I ni 67,696 sawa na asilimia 54.09 na daraja la pili ni watahiniwa 43,515 sawa na asilimia 34.77.

Matokeo hayo ya mtihani wa kidato cha sita na mtihani wa ualimu uliofanyika Mei 2026 yametangazwa leo Jumatatu, Julai 6, 2026 jijini Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa Necta, Profesa Said Mohammed.

"Mwaka 2025 watahiniwa waliopata madaraja 1-3 walikuwa 125,375 sawa na asilimia 99.62 huku asilimia 48.57 wakipata daraja la kwanza na asilimia 49.24 wakipata daraja la II hivyo kiwango cha ufaulu kimeendelea kuwa cha juu mwaka 2026,” amesema.


Endelea kufuatilia Mwananchi…