Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ngono umri mdogo yatajwa kuchangia saratani shingo ya kizazi

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya saratani kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), Dk Nanzoke Mvungi

Muktasari:

Imeelezwa kuwa kushiriki ngono katika umri mdogo kunawaweka wasichana hatarini kupata saratani ya shingo ya kizazi.

Dar es Salaam. Imeelezwa kuwa kushiriki ngono katika umri mdogo kunawaweka wasichana hatarini kupata saratani ya shingo ya kizazi.

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam jana na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya saratani kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), Dk Nanzoke Mvungi wakati wa mkutano wa kuwajengea uwezo wanawake kuhusiana na magonjwa ya saratani ya shingo ya kizazi na matiti ulioandaliwa na Hospitali ya Massana.

Alisema wanawake pia katika kujikinga na magonjwa hayo wanashauriwa kufanya uchunguzi wa awali wa saratani hizo, hatua itakayosaidia kugundua tatizo mapema na kulitibu.

“Ni muhimu kwa wanawake kufanya uchunguzi wa saratani ya kizazi, hata kama wameacha kujamiiana maishani mwao na hata kama hawakuwahi kukutwa na mabadiliko ya awali ya saratani hiyo katika uchunguzi uliopita,” alisema

Alisema aina hizo za saratani zinakua kwa kasi hapa nchini ikilinganishwa na miaka ya nyuma, huku takwimu zikionyesha saratani inayoongoza kwa wanawake ni ya shingo ya kizazi kwa asilimia 33, ikifuatiwa na saratani ya matiti ambayo ni asilimia 12.

Alisisitiza kuwa watoto wa kike wanaoanzia miaka tisa kabla hawajaanza kujishiriki katika ngono wanatakiwa kupata chanjo, kwa kuwa kirusi kinachoeneza saratani ya shingo ya kizazi kinaweza kudhibitiwa na chanjo inayotolewa na Ocean Road.

“Utoaji chanjo ulianza Wilaya ya Hai, Moshi kwa wanafunzi wote waliokuwa shule za msingi, ni matumaini yangu kuwa litakuwa endelevu, tukiweza kufanikiwa kuwachanja watoto wetu tutautokomeza ugonjwa huu katika nchi yetu,” alisema.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Tiba wa Hospitali ya Massana, Dk Robert Josiah alisema wamewamua kutoa elimu hiyo baada ya kubaini kuwepo kwa wanawake wengi wanasumbuliwa na saratani ya shingo ya kizazi na matiti huku wengi wao wakishindwa kupata tiba kwa kukosa elimu sahihi.