Ni Profesa Mkenda wa CCM jimbo la Rombo

Muktasari:

Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Rombo, Godwin Chacha amemtangaza mgombea ubunge wa CCM jimbo la Rombo, Profesa Adolf Mkenda kuwa mshindi baada ya kupata kura 48,122 kati ya kura  61,111 zilizopigwa.

Rombo. Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Rombo, Godwin Chacha amemtangaza mgombea ubunge wa CCM jimbo la Rombo, Profesa Adolf Mkenda kuwa mshindi baada ya kupata kura 48,122 kati ya kura  61,111 zilizopigwa.

Mgombea wa Chadema, Patrick Asenga amepata kura 9,519, Jafet Masawe wa ACT- Wazalendo kura 1,564, Joseph Selasini wa NCCR Mageuzi  kura 416,  Michael Clemence  (TLP) kura 167 huku Jubilate Tadayo (CUF) akipata kura 107.

Akitangaza matokeo hayo leo Alhamisi Oktoba 29,2020, Chacha amesema waliojiandikisha ni 146,170,waliopiga kura ni 61,111, kura halali ni 59,895 huku kura zilizoharibika zikiwa  1,216

Akizungumza baada ya kutangazwa, Mkenda amesema atahakikisha wananchi wa jimbo hilo wanapata maendeleo.