Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

NIDA yawataka wananchi kuchukua vitambulisho vya Taifa

Mkurugenzi wa Idara ya Uzalishaji wa Vitambulisho vya Taifa wa NIDA, Edson Guyai akizungumza na wananchi wa Temeke, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Utambulisho Duniani yaliyofanyika katika ofisi za mamlaka hiyo wilayani humo.

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa NIDA imefanikiwa kuandikisha Watanzania milioni 26 kati ya milioni 31 wenye umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea, kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya 2022.

Dar es Salaam. Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imewataka Watanzania waliojiandikisha kuchukua vitambulisho vyao, ikisisitiza kuwa nyaraka hiyo sasa ni muhimu kwa kila mwenye umri kuanzia miaka 18.

Kauli hiyo imetolewa jana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, George Seni, alipokuwa akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo katika maadhimisho ya Siku ya Utambulisho Duniani yaliyofanyika kitaifa katika ofisi za NIDA, Wilaya ya Temeke.

Seni amesema licha ya mamlaka hiyo kutoa tangazo la mwisho wa kuchukua vitambulisho kufikia Juni mwaka huu, wananchi wengi bado hawajafanya hivyo, jambo lililosababisha baadhi ya namba za simu kufungiwa.

“Natoa rai kwa wananchi hususan wale waliopokea ujumbe mfupi wa maandishi kwenye simu zao, kufika katika ofisi walizojisajilia ili kupata vitambulisho vyao,” amesema.

Akizungumzia maadhimisho hayo, Seni amesema NIDA imeyatumia kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kitambulisho cha Taifa sambamba na kutoa huduma mbalimbali kwa wakazi wa Temeke.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Uzalishaji wa Vitambulisho NIDA, Edson Guyai amesema hadi sasa mamlaka hiyo imefanikiwa kuandikisha Watanzania milioni 26 kati ya milioni 31 wenye umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea, kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya 2022.

“NIDA ipo kwa ajili ya kuhudumia Watanzania wote ili kuhakikisha ifikapo mwaka 2030 kila mmoja awe amejiandikisha na kuwa na kitambulisho cha Taifa,” amesema Guyai.

Maadhimisho ya Siku ya Utambulisho Duniani mwaka huu yamefanyika kwa mara ya saba tangu kuanzishwa na taasisi ya ID for Africa, yakiongozwa na kaulimbiu isemayo: “Utambulisho Wangu, Mwanvuli Wangu” ikiwa na lengo la kuonyesha umuhimu wa kuwa na kitambulisho cha Taifa.