Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Njia sahihi za kusafisha sehemu nyeti za uzazi

Muktasari:

  • Kuna wanawake wanaojipenda na kuwa wasafi kimwili ikiwamo maeneo ya uzazi.

Kuna wanawake wanaojipenda na kuwa wasafi kimwili ikiwamo maeneo ya uzazi.

Wapo wanaobeba maelekezo potofu ya mtaani na kufanya usafi eneo hilo kwa kuingiza ukeni vitu kama sabuni, maji yenye kasi, manukato, dawa ya kuoshea na kuulia vimelea anticeptic, vilainishi na mitishamba.

Baadhi huamini kufanya hivyo ndiyo usafi salama wakujikinga na maradhi kama fangasi ukeni, magonjwa yanayoenea kwa kujamiiana na kuondoa harufu mbaya.

Ukweli ni kwamba, njia hizi si salama kwa afya ya uzazi kwa kuwa, vitu hivi kuviingiza ukeni vinasababisha mabadiliko ya njia hivyo na hatimaye kuharibu mfumo wake wakujilinda.

Na haishauriwi kuweka manukato kukata harufu kwa kuwa harufu asili ya ukeni huongeza usisimkaji kwa mwenza wa kiume.

Sayansi ya kitabibu kwa magonjwa ya kinamama inathibitisha uingizaji vitu hivyo ukeni kunaharibu mfumo wa kinga ikiwamo tindikali ya ukeni na kuua vijidudu rafiki.

Kwa kawaida ukeni huwa na vijidudu rafiki ambao ni bakteria na fangasi ambao huwadhibiti vijidudu visivyo rafiki.

Njia ya uzazi ya kiasili ya kujisafisha ambao ni ute ute mweupe ulio na harufu ya kiasili unaoshuka kila siku kutokea katika shingo ya uzazi.

Ni kawaida ute huo unaweza kuwa kiasi cha kijiko cha chai kubadilika badilika ikiwamo pale kijiyai kinapopevushwa ute huo huwa mzito na rangi ya kahawia iliyofifia.

Endapo ute huo utakuwa na harufu mbaya kama kitu kilichooza au uvundo mzito kama shombo la samaki kuenda ni ishara ya magonjwa, hivyo vizuri kufika katika huduma za afya. Zipo njia salama kiafya zikitumika husaidia kuboresha mfumo wa ulinzi dhidi ya vimelea adui wanaovamia njia hiyo.

Kitabibu inashauriwa mwanamke asiingize kitu chochote ukeni, inatakiwa kuoga na kusafisha maeneo hayo kwa maji ambayo ni safi na salama na kutumia sabuni bila kuingiza ukeni.

Mwandishi wa makala haya ni daktari wa binadamu

DK SHITA SAMWEL