Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Norway kupiga marufuku mitandao ya kijamii kwa watoto chini ya miaka 16

Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Hatua hiyo inaifanya Norway kuungana na mataifa mengine duniani yaliyoanza kuchukua hatua kali kudhibiti matumizi ya teknolojia kwa watoto.

Norway. Serikali ya Norway imetangaza mpango wa kuwasilisha muswada bungeni utakaopiga marufuku watoto walio chini ya umri wa miaka 16 kutumia mitandao ya kijamii, hatua inayolenga kulinda ustawi wa watoto katika ulimwengu wa kidijitali.

Kwa mujibu wa tovuti ya habari ya ABC News hatua hiyo itakayowasilishwa bungeni kabla ya mwisho wa mwaka 2026, inaifanya Norway kuungana na mataifa kadhaa yaliyoanza kuchukua hatua kali kudhibiti matumizi ya teknolojia kwa watoto.

Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Jonas Gahr Støre akizungumza na vyombo vya habari leo Aprili 24, 2026 amesema lengo la sheria hiyo ni kuhakikisha watoto wanapata malezi yanayozingatia ukuaji wao wa kawaida bila kuathiriwa na matumizi makubwa ya mitandao.

“Tunalenga kurejesha utoto wa watoto wetu. Michezo, urafiki na maisha ya kawaida ya kila siku ya watoto.”

Mpango huo unafuatia hatua kama hiyo iliyochukuliwa na Australia, ambayo mwaka jana ilipiga marufuku matumizi ya mitandao ya kijamii kwa watoto chini ya miaka 16.

Wakati huo huo, bunge la Uturuki limepitisha sheria inayokataza watoto chini ya miaka 15 kutumia mitandao hiyo, huku pia likizihusisha kampuni za michezo ya kidijitali.

Nchi nyingine za Ulaya zikiwamo Denmark, Ufaransa na Hispania nazo zimeanza kuchukua hatua au kuandaa sheria zinazolenga kudhibiti matumizi ya mitandao kwa watoto.

Kwa mujibu wa Serikali ya Norway, jukumu la kuthibitisha umri wa watumiaji litawekwa mikononi mwa kampuni za teknolojia, ingawa haijabainishwa ni majukwaa gani yatakayoathiriwa moja kwa moja.

Hatua hizi zinachukuliwa wakati dunia ikiendelea kujadili athari za matumizi ya mitandao ya kijamii kwa afya ya akili, tabia na maendeleo ya watoto.